Sanaa ya Tanzania hasa muziki na filamu kuna hela nyingi sana iko wazi wasanii wanashindwa kuitumia.Inauzunisha sana unaposikia msanii anasema sanaa ya bongo hailipi inakupa hela ya mboga.Hizi ni kauli za wasanii wanaoshindwa kufikilia na kuwa na mawazo mgando.Baadhi ya mambo hayaitaji kufanywa na serikali wasanii wenyewe wana uwanja mkubwa wa kurekebisha.
BRANDING,msanii ni bidhaa kubwa endapo atajitambua yeye ni bidhaa kama zilivyo soda,nguo na viatu.Jina kama Lady J dee,Ben Paul au Wema sepetu,Linapotajwa tu nchini kuna kitu akilini mwetu kina click.Hii inadhihilisha ndani ya hilo jina kuna kitu ndani yake.Msanii pekee aliyeweza kujibrand nchini nakufanikiwa ni Diamond Platnum.Sio kwamba huyu bro anatoa nyimbo kali ila ile brand yake inambebe kutajwa tu nyimbo ya Diamond watu wana hamu ya kutaka kuisikia.Unakuta msanii wa Tanzania anajiita Angelina Joel wa bongo serious unakuzaje jina la mwezako.Hujawahi kukuta hoteli Tanzania inajiita nakujifananisha na hoteli za Ulaya.
PROMOTION ya bidhaa za wasanii bongo ni shida ukitoa wachache wenye uthubutu wengine nikisanga,Kila msanii wa bongo fleva bongo anaamini redio moja tu inaweza kumtoa kimuziki,Wasanii wanaijua wote inapatikana mikocheni.Sasa ndugu masanii nchi nzima itakujua kupitia redio moja.Nguvu zote za msanii anaamishia kituo cha redio kimoja.Sehemu kama Itune na Vevo kazi huingiza hela lakini hadi star wetu bongo hayupo huku Ben Paul pekee ndo anapatikana Itune.J Zay hadi kesho redio za mitaani anaziheshimu akiitwa kwa mahojiano anaenda sababu zilimfanya ajulikane.
CONNECTION wasanii bongo hawatafuti kujikuza kwakufanya kazi na wanamuziki wa nje.Wachache wameweza na wanapiga bao nawanahesabika.Msanii kutenga fedha na kwenda Nigeria kutafuta kufanya kazi na wasani wa huko ili kutanua soko inakua shida.Shetta kwa sasa ni habari ya nchini na nje ya nchi,wasanii wamekalia kujiita habari ya mujini na hana jipya kwenye tasnia.
SOKO wasanii hawalitumii inavyobidi nikuridhika ingali kazi zao zinapendwa dunia nzima.Bongo movie inatazamwa Africa zaidi ya nchi kumi,Uliza filamu zao zinakouzwa utasikia iyo kazi ya msambazaji,Sasa filamu unacheza wewe jina kubwa unalipwa million mbili wakati filamu ikiuzwa kwa buku kwa nakala milioni mbili unapata bilioni mbili.Idadi ya watu wa Dar es Salaam ni milioni tano watu wakununua kazi milioni mbili hawafiki hata nusu yake.Wasanii bongo unaitaji mpitishiwe le umemezz vichwani.
Wasanii wanaolalamikiwa wana vipaji ila hawatoki wanabaniwa hawapo wanapotakiwa ni hawa Belle 9,Rama D,Enika,Tid,Q chiller ,One Incredible,Nikki Mbishi na Grace matata.Katika dhana halisia wamefanya kipi kwenye mziki upande wa kujitafutia soko,connection,kuji brand na nidhamu zao.
Sanaa ya bongo ilipofika msanii fanya kazi nzuri studio tafuta proffessinal wa masoko wakufanyie kazi zako.Babu Tale na Said Fela wasanii wao wanafanya vizuri sokoni sio kwamba wanaimba sana ila wasimamizi wao wanajituma na kufanya kazi kwa ufanisi.
0 comments:
Post a Comment