Today 10:52
Senior Member - Jamiiforums
Wakati mchakato wa uteuzi ndani ya CCM ukielekea ukingoni,mwenyekiti wa UWT Taifa,mhe. S. Simba amempelekea ujumbe mzito Mhe. Kikwete kuwa wanawake wa Tanzania wamemtuma kuwa chaguo lao ni Lowassa hivyo basi akiwapelekea mtu mwingine tofauti hawatampa kura zao.
Wakati huo huo mwenyekiti wa UVCCM Taifa naye akapeleka ujumbe kuwa vijana wa Tanzania chaguo lao ni Lowassa na wakiwapelekea mtu tofauti, basi wao wasilaumiwe kwa kitakachotokea,walipoulizwa msimamo wao ni upi wakajibu haraka kuwa wao wanawakilisha ujumbe wa watu wao.
Ikabidi aitwe pia Bulembo aulizwe kama naye ana ujumbe wa wazazi, yeye akajibu kwa jazba kuwa haya makundi yatakiharibu chama,akauliza wenzake wa vijana na wanawake walikaa lini,wapi na wajumbe wao? akashauri kuwa bora Lowassa na Membe waondolewe kwenye mchakato abaki Pinda.
Hapo akashambuiwa kuwa hoja yake ina lengo la kumpigia mtu debe sio kunusuru chama.Kuna baadhi ya wazee waliitwa kutoa ushauri ila walisikitishwa na kauli za mzee Kingunge kuwa anatumika kumtisha Mwenyekiti.Vimepangwa vikao kadhaa na watu tofauti ili kufikia muafaka kabla ya kuanza vikao vya maamuzi na imeazimiwa wagombea wahusishwe pia katika kukinusuru chama.Ratiba ya vikao vya uteuzi inaweza kusogezwa tena mbele kama maridhiano yatachelewa nje vikao.
Source: Jikoni(Jumuiya ya wazazi CCM Taifa)
0 comments:
Post a Comment