Posted by Williammalecela.com on Friday, July 10, 2015
Rose Muhando: Nafikiria kurudi kwenye Uislamu
NYOTA
wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema
alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo
zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi
katika imani yake ya kwanza.
Akizungumza na
Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo
tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.
Pia Rose alikwenda
mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu
kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.
“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.
“Mfano, mtu
anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa
taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata
jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata
faraja,” alisema Rose.
Mwimbaji huyo
amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa
ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.
Chanzo: GPL
0 comments:
Post a Comment