Ujue mwenzenu, kila kukicha naendelea kufurahishwa na utitiri wa marafiki zangu waliohamasika kuwania nafasi za ubunge wa jamhuri ya Muungano. Lakini jana usiku baada ya kutafakari sana nikajikuta nimejiuliza tu, ina maana hawa wote wana majibu ya changamoto zinazotukabili huku mtaani, au wanaenda kufanya nini bungeni? Wote wana uchungu na nchi na ni wapenda mabadiliko, au wanaenda kuwa wasikilizaji kama ambao tuliwaamini kabla? Mimi ninawamudu watano tu, hawa wengine nawaona ona tu, ila kiukweli nategemea aina ya vijana itakayoingia bungeni kwenda kuishauri serikali masuluhisho ya changamoto zinazoikabili sio kuingia kule nao kuchukua posho na kuilaumu serikali, aina hii ya wabunge, itazidi kuididimiza nchi. Sasa hivi, tuna wabunge walalamishi wengi, kuliko watoa majawabu ya changamoto. Cha kusikitisha sasa wengi wao ni vijana. Kila siku wao watu wa kulipua mabomu yanayozidi kutuchanganya sisi wa hali ya chini tunaoishi kwa kipato cha dola moja. Halaf sasa wabunge hawa mastaa majimboni mwao migogoro kibao! Naitamani aina mpya ya viongozi vijana ambao watajenga nchi yetu bila kujali itikadi zao. Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment