Posted by Williammalecela.com on Wednesday, August 19, 2015
 |
Baada
ya Magazeti kadhaa leo kuandika habari kuwa chama cha Democrasia na
maendeleo chadema kimepanga kuzindulia kampeni zake za uchaguzi katika
uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam hatimaye serikali imeibuka na
kupiga marufuku matumizi ya uwanja huo kwa kile walichosema kuwa sio
matumizi ya uwanja huo.
Akizungumza na wanahabari muda huu Jijini
Mkurugenzi wa idara ya Habari maelezo Bwana ASSA MWAMBENE (pichani)
Amesema kuwa ni kweli walipokea maombi kutoka CHADEMA tarehe 12 mwezi wa
nane ya kuomba kutumia uwanja wa taifa mpya kwa ajili ya kuzindua
kampeni na Tayari wameshawajibu kuwa hawawezi kuruhusu uwanja wa
serikali kutumika kwa shughuli za kisiasa kwa chama chochote nchini.
Amesema
kuwa wameshangaa kuona Taarifa mbalimbali kwenye magazeti leo zikisema
kuwa kampeni ya CHADEMA itazinduliwa hapo wakati tayari serikali
imeshapiga marufuku sehemu za serikali kutumika katika shughuli za
kisiasa. |
0 comments:
Post a Comment