"Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto
• Gari la Ole Sendeka lavunjwa vioo,Ole Nangoro anusurika kichapo
• Nyumba yake yavamiwa na wanachama, wavunja taa na kumpiga mlinzi
Na. Mohamed Hamad Manyara
JESHI la polisi wilayani Kiteto mkoani Manyara limetumia mabomu ya
machozi na silaha za moto kuokoa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto
Benedict Ole Nangoro na Christopher Ole Sendeka pamoja na kamati ya
siasa ya Mkoa wa Manyara waliofika kuhakiki matokeo ya Ubunge
Awali wajumbe hao walizuiwa kwa mawe na magogo barabarani kata ya
Engusero wasifike makao makuu ya wilaya ya Kiteto wakitokea Dodoma, hali
iliyolazimu Jeshi la Polisi kuwaokoa kwa kuwapa ulinzi kwa kuwafikisha
Kibaya kwaajili ya kuhakiki matokeo hayo
Baada ya kamati ya siasa
ya mkoa kufika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto majira ya mchana
walianza kuhakiki matokeo ya Ubunge ambayo yalidaiwa kulalamikiwa na
aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro aliyeambatana
na wajumbe hao kutaka yahakikiwe
“Baada ya kusikia kuna kamati ya
siasa mkoa wa Manyara imefika wanachama tulilazimika kufika ofisi za
CCM kutaka kujua hatma ya ujio wao, kwani tumeshuhudia maeneo mengi
matokeo ya uchaguzi yanabadilishwa baada ya kutangazwa washindi”alisema
mwananchi Rajabu Jagon"
0 comments:
Post a Comment