Musa Mateja
Aah!
Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati
alijikuta akipigwa butwaa kufuatia kitendo cha mcheza shoo wake, Moses
Iyobo ëMozeí na mzazi mwenzake, Aunt Ezekiel kuoneshana ‘mahaba nipeleke
kuzimu’ hadharani, Risasi Mchanganyiko lilikuwepo kushuhudia.
Tukio
hilo la Diamond kupagawishwa na mahaba ya wawili hao lilijiri usiku wa
kuamkia Agosti 3, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Regency iliyopo
Mikocheni jijini Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ‘bethidei’
ya Iyobo. Lakini kabla ya kufika kwenye tukio hilo, twende hatua kwa
hatua.
MWONEKANO WA DIAMOND UKUMBINI
Akiwa
kwenye sherehe hiyo iliyojazwa pia na mastaa, muda mwingi Diamond
alionekana mwenye furaha ya hali ya juu kufuatia mishemishe za bethidei
hiyo iliyoandaliwa na Aunt kama moja ya kumshtukiza ‘sapraizi’ mpenzi
wake huyo.
Habari zinasema mpaka Iyobo anaingia ukumbini hapo alikuwa hafahamu kama kuna sherehe ya kuzaliwa kwake.
Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kabeba keki.
MUDA WA MSHTUKO
Iyobo alizama ukumbini hapo saa 7 usiku kwa kuitwa na Aunt. Aunt pia ni staa wa sinema za Kibongo.
Baada
ya Iyobo kuingia ukumbini alipata mshtuko kufuatia Diamond na nyota wa
filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kumkaribisha kwa kummwagia maji na
vinywaji mbalimbali ambapo waalikwa wengine nao waliungana kumuogesha
huku wakimwimbia ‘hepi bethidei tu yu.’
DIAMOND AFUNGUA SHAMPENI
Baada
ya zoezi la kumkaribisha Iyobo aliyekuwa amelala zake nyumbani kwa Aunt
kumalizika, Diamond alipewa chupa ya kinywaji aina ya shampeni kwa
ajili ya kufungulia sherehe hiyo ambayo ilianza hapo.
Moses Iyobo akiwa kamkumbatia mpenzi wake Aunt Ezekiel.
DIAMOND ACHEZA HUKU NA KULE
Katika
hatua nyingine, waalikwa walitumbua macho kumwangalia Diamond ambaye
muda mwingi alikuwa akicheza tena kwa vituko mbalimbali.
ABEBA KEKI
Pengine
ni kwa sababu ilikuwa bethidei ya mcheza shoo wake, kwani ulipofika
wakati wa kupeleka keki mezani, Diamond aliibeba yeye hadi eneo husika
kwa ajili ya ‘kulishania’.
MAHABA NIPELEKE KUZIMU SASA!
Sasa
wakati Aunt na Iyobo wakiwa katika tukio la kulishana keki kwa mtindo
wa mahaba nipeleke kuzimu (mdomo kwa mdomo), Diamond alionekana kushtuka
na kuwatumbulia macho (angalia picha ukurasa wa mbele).
Diamond
aliendelea kuwatumbulia macho kama anayewachungulia huku akipanua mdomo
kwa mshangao ambapo wawili hao wala kiroho hakikuwadunda kwamba wapo
laivu.
KUMBE IYOBO ALIFUNDISHWA
Baada
ya kuwashangaa wawili hao kwa karibia sekunde kadhaa, Diamond aliibuka
na kusema kuwa, kulishana keki wawili hao kwa staili hiyo, ndivyo WCB
ilivyomfundisha Iyobo kwamba, anapokuwa na mpenzi wake huyo sharti
amlishe kwa kinywa na si kutumia uma.
DIAMOND HAWEZI KUFANYA HIVI
Jambo
ambalo lilijitokeza kwenye sherehe hiyo ambapo waalikwa walisema katu,
Diamond hawezi kulifanya hivyo kwenye sherehe nyingine (mbali na
jukwaani) ni kitendo chake cha kuimba zaidi ya nyimbo zake tano ukiwemo
Nana unaotamba kwa sasa. Huwa akialikwa mahali, Diamond huimba wimbo
mmoja au mbili tu.
Hata
hivyo, Diamond mwenyewe alisema kuimba nyimbo zote hizo na kuruhusu
waalikwa kucheza ni moja ya kuonesha upendo na hamasa yake kwa Iyobo
kwani bila yeye hakuna Diamond wala WCB kwa jumla.
USIRI WA UMRI KAMA KAWAIDA
Hata
hivyo, kama kawaida, mpaka mwisho wa shughuli hiyo, haikuelezwa wazi
kwamba, Iyobo alikuwa akisherehekea kutimiza miaka mingapi ya kuzaliwa
kwake zaidi ya kusemwa; ametimiza miaka kadhaa!
0 comments:
Post a Comment