Mke wa msanii wa muziki, H.Baba, Flora Mvungi amesema anajipanga kuongeza watoto wawili wengine ili atimize malengo yake wa kuwa na watoto wanne.Flora ameiambia Bongo5 kuwa Mungu akimjalia atazaa watoto wengine wawili kwa haraka ili kutimiza malengo yake.
“Nawapenda sana watoto wangu wawili (Tanzanite na Africa) napumzika kidogo halafu nataka nitafute wawili wa fasta,” amesema. “Mpango wangu ni kuwa na watoto wanne, kwahiyo tumuombe Mungu alisimamie hili litimie,” ameongeza.
Muigizaji huyo amesema mtoto wake Tanzanite anaonesha kila dalili ya kuja kuwa mwanamuziki mzuri.
“Tanzanite interest yake kubwa ni muziki, sema sasa hivi ndio ana miaka miwili na tunataka kumkazia kwanza asome ndio tumwingize kwenye muziki.”
-Bongo5
0 comments:
Post a Comment