Posted by Williammalecela.com on Monday, August 31, 2015

Mwandishi wetu
Acha
kabisa! Baadhi ya mastaa wa sinema na muziki Bongo, wamejiachia na
kujikuta wakikata mauno mbele ya Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
aliyekuwa mgeni rasmi aliyeambatana na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.
Asha-Rose Migiro hali iliyozua minong’ono kwa waalikwa.
Tukio
hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilijiri usiku wikiendi
iliyopita kwenye Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro ambapo kulikuwa
na uzinduzi wa Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao iliyoandaliwa na
kusimamiwa na Msanii Wema Isaac Sepetu na Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’.
Mwenyekiti
wa kampeni hiyo, Steve Nyerere alianza kwa kuzungumzia lengo la Mama
Ongea na Mwanao ni kuhakikisha kila mwanamama anaongea na mwanaye juu ya
kupiga kura kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka
huu.
“Tutahakikisha
kampeni hii inafika nyumba hadi nyumba, chumba hadi chumba ili kuona
kila mzazi, hasa mama anaongea na mwanaye kwa sababu wanawake wana fursa
kubwa ya kuongea na vijana wao na kuwahamasisha kupiga kura,” alisema
Steve.
“Mimi
kama kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) najua ziwa la mama ni tamu na
haliishi hamu, kampeni hii ina lengo la kufanya uamuzi na mabadiliko
kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 hivyo kwa pamoja tunasema ushindi
kwetu ni lazima,” alisema Wema ambaye ni makamu mwenyekiti wa kampeni
hiyo.
Kwa
upande wake JK alianza kwa kuwatoa hofu wasanii waliokatwa kwenye kura
za maoni na kuwaambia kuwa yeye alianzia hukohuko walikoanzia wao hivyo
wasikate tamaa.
“Nakumbuka mwaka 1995 na mimi nilikatwa lakini sikukata tamaa hadi 2005,” alisema JK akiunga mkono kampeni hiyo.
Baada
ya uzinduzi huo, wasanii walimpa tuzo JK ambayo iliambatana na picha ya
mke wake, Mama Salma Kikwete iliyotokana na kuiongoza vyema nchi hii na
kumtakia mapumziko mema huku Migiro naye akipewa tuzo kisha wasanii
wakaanza kula, kunywa na kukata mauno mbele ya kiongozi huyo wa nchi.
Imeandikwa na Shani Ramadhani, Musa Mateja na Imelda Mtema.
0 comments:
Post a Comment