Friday, August 28, 2015



SUMAYE ALIISHAKATALIWA TOKEA ZAMANI…


Waziri Mkuu wa zamani, kwa miaka 10, Frederick Sumaye amejiondoa CCM na kujiunga na UKAWA, sio siri kuwa akiwa Waziri Mkuu wa CCM boss wake alikuwa akimuita Mr. Zero. na kutoka kwake  ni muendelezo wa kuhakikisha rais wa mwaka huu anatoka Kaskazini. Hii ni ukichukulia viongozi wengi wa UKAWA ni wa Kaskazini.

  Frederick Sumaye alikuwa ni hasimu mkubwa wa Lowassa tokea kwenye kinyang’anyiro kilichomuingiza JK madarakani mwaka 2005. Kipindi hicho Lowassa ndio alikuwa mwenyekiti wa mtandao na timu ya kampeni iliyomuingiza JK madarakani.

Fredrick Sumaye mwaka huo (2005) alitamka “Mgombea urais anayetumia kalamu kuchagua wenzake kuingia Ikulu, atatumia risasi kujisafishia njia”. Mwaka huu 2015, alisema iwapo CCM itampitisha mtuhumiwa mkuu wa ufisadi kuwa mgombea urais, atajiondoa CCM.

Uhasama wao umeisha kutokana na wote KUKATWA kwenye mchakato wa urais wa CCM. Lakini suala la u-kaskazini limewaunganisha na kuwafanya wasahau tofauti zao.

Frederick Sumaye alishakataliwa tokea zamani. Mwaka 2005 kwenye mchakato wa ndani ya CCM wa kutafuta mgombea urais, aliishia kuwa wa 4 kwenye kura nyuma ya Jakaya Kikwete, Salim Ahmed Salim na Prof Mark Mwandosya. Ni nadra sana, kwa mtu ambaye ni waziri mkuu (katika kipindi bado akiwa waziri mkuu) kushindwa kufika tatu bora. Hii inaonyesha kutokubalika kwa hali ya juu. Afadhali angekuwa amekatwa.

Mwaka 2012, kwenye uchaguzi wa kutafuta wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya NEC ya CCM kwa kupitia jimbo la Hanang, alishindwa na mama Mary Nagu. Mwaka 2015 jina lake halikufika kwenye 5 bora ya CCM. LILIKATWA!

Huyu ni mmoja ya watu wanaohamia UKAWA wakitegemewa kuleta MABADILIKO kama ni kweli something is a miss.

- Waziri Mkuu wa kwanza Tanzania kusika nafasi hiyo kwa miaka 10 mfululizo leo anatafuta urais UKAWA kuna nini alisahau kukibadilisha kwenye miaka 10 ya utawala wake? I mean it is a Democracy ni haki ya kila mwananchi kuamua na kuamini anachotaka lakini at some point sujiulize maswali serious kuhusu integrity ya Viongozi wanaohamia UKAWA kutoka CCM are they genuine? Hivi ni kweli UKOMBOZI unaweza kuletwa na Sumaye na Lowasa? Seriously? Ni maswali Wananchi tunatakiwa kutafakari kabla ya kupiga piga makelele na kukimbizwa kwenye mikutano ya kampeni hivi ni kweli hawa Viongozi watabaki UKAWA ikishindwa kushika Dola? Watauziwa na nini kurudi CCM kama walivyohama? 

- WATANZANIA TUWENI MACHO SANA!!

Le Mutuz Nation 28/8/2015

0 comments:

Post a Comment