Tuesday, August 25, 2015

Angalia picha hii kwa umakini huyu ni Lowassa anayengangania kwenda IKULU. 
Picha hii inatusaidia sana kufanya justification ya ugonjwa wa Lowassa. 

Kwenye picha hii anaonekana akishuka kwenye Costa lakini Mazingira aliyopo ni kushindwa kabisa kushuka ngazi za gari kabisa angalia mambo yafuatayo:-


1. Kuna mtu kamshika kichwa kwa Nyuma kumpinda ili uweze kuendana na kimo cha mlango. Inamaana akili yake haiwezi tena kukadiria vitu vilivyopo mbele yake. Hili ni tatizo kubwa mtu anaona mbili anasema moja na ndio maana pamoja na udhaifu alionao bado akili imeahindwa kutafsiri kuwa atashindwa. 

2. Kikawaida mtu anayeshuka kwenye ngazi mwenye Afya njema hushuka mwenyewe bila kujishika mahali ni mara chache sana kama mtu akihitaji msaada hutumia mkono mmoja. Angalia Mikono yake yote imejishika kwenye chuma za gari. Hili ni tatizo huna haja ya kuwa daktari ufahamu hili.

3. Chini kuna mtu kanyoosha mkono anataka Lowasa ajiamini aachie mkono wa kulia ampatie ila akili imegoma kwa kuwa unajua ukubwa wa tatizo alilonalo Mh.

Hivii kwa nn jana badala ya kwenda location ya Igizo hakupitia hospital? 

Chagua MAGUFULI achana na hawa watu.

Ole Mushi




0 comments:

Post a Comment