2. Nimeamua kujitokeza leo hii ili kumesha upotoshaji na kuuweka wazi ukweli.
3.Sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia ninachokiamini.
4.Sina ugomvi na kiongozi yeyote maana siasa sio uadai.
6. Naweka wazi kuwa mimi sikuwa likizo na hakuna aliyenipa likizo yoyote.
7.Kilichotokea
ni kuwa niliamua kuachana na siasa tangu 28.7.2015 saa sita
usiku baada ya kutoridhishwa na kilichokuwa kinaendelea ndani
ya chama changu.
8.Ni kweli nilishiriki kumleta Lowassa CHADEMA Lakini nilikuwa na misimamo yangu ambayo ilitufanya tusielewane.
9.
Baada ya Lowassa kukatwa pale Dodoma, Gwajima ambaye ni
mshenga wa Lowassa alinipigia simu kutaka kujua nii cha
kufanya.
10. Nilimpigia Mwenyekiti Mbowe kumjulisha na tukakubaliana kupanga muda wa kuwasikiliza.
11.
Kabla ya kuanza kuwasikiliza, msimamo wangu ulikuwa ni kumtaka
Lowassa kwanza atangaze kuhama chama, aweke wazi ni chama gani
anaenda na ajisafishe juu ya tuhuma zake
12.Tangu
akatwe jina, Lowassa hakutangaza kujitoa CCM na wala
hakujisafisha na tuhuma zake, kitu kilichonifanye nitofautiane
naye.
13. Niliwauliza wanachadema wenzangu kuwa Lowassa anakuja kama Mtaji au Mzigo?
14.
Swala sio urais kama watu wanavyozusha, mimi nilikuwa nataka
mgombea mwenye uwezo na sifa ambaye ataweza kuitoa CCM. Sikuwa
na tamaa ya urais kama watu wanavyosema
15.
Tangu Gwajima atupe taarifa za ujio wa Lowassa, Swali langu
la Lowasssa kuwa Mtaji au mzigo halikuwahi kujibiwa.
16. Nilitaka kujua ni mtaji gani lowassa atakuja nao na ni viongozi gan atakuja nao.
17. Nilijibiwa kuwa anakuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa wilaya.
18.Baada
ya ahadi hiyo, nilitaka sasa nipewe majina ya hawa watu
lakini mpaka tarehe 25 july sikupewa hayo majina
19.
Wenzangu waliniambia kuwa tarehe 27 niitishe kikao cha dharura
ila niligoma kwa sababu nilikuwa sijapewa haya majina
20.
Ndani ya kikao hicho, tulianza kwa mabishano makali kati
yangu na Mbowe, Lissu na Gwajima, viongozi wenzangu ni shahidi
na mungu anajua. Msimamo wangu ulikuwa ni uleule kujua mchango
wa Lowassa
21.
Kikao kile kikavunjika, baadae tukaingia kamati kuu lakini bado
msimamo wangu ulikuwa ni uleule. Baadae nikaandika barua ya
kujiuzulu.
22.Profesa Safari aliichana ile barua.
23.Cha
kusikitisha ni kuwa Kesho yake picha zikaanza kusambaa
mtandaoni zikimuonyesha la lowassa japo viongozi wangu
walizikana zile picha. Kibaya ni kuwa viongozi waliuficha
ukweli
24. Kesho yake niliandika tena barua rasmi ya kujiuzulu.
25. Baada ya pale zikaanza propaganda za uongo zikimuhusisha hadi mke wangu eti kanizuia.
26.
Naomba watanzania wajue kuwa mke wangu hakuwahi kunizuia kwa
lolote, lkn hata angefanya hivyo sio mbaya maana hata yeye ni
mwanaharakati mwenye uchungu na nchi hii.
27.
Mke wangu aliwahi hadi kuumia wakati akipigania ukombozi wa
nchi hii.....Lakini sio mbaya, familia yangu imezoea propaganda.
28.
Kikubwa katika harakati ni credibility ambayo lazima uilinde
na mimi sitaki jina langu liharibiwe na ni haki yangu.
29. Maslah mapana ya taifa ndiyo yaliyotufikisha hapa na sio maslahi binafsi.
30.Lowassa na wapambe wake ni waongo maana hakuna hata kipengele kimoja walichokitekeleza.
31. Tulitaka hao wabunge 50 waje kwanza kabla ya mchato wa uteuzi ccm
32. Napinga kuchukua makapi ya CCM kuyaita MTAJI.
33.Mtu kama Sumaye ni FISADI na nilikuwa siongei naye
34. Sumaye aliwahi kusema CCM wakimchagua Lowassa atahama chama. Leo Lowassa kawaje msafi??
35. Tulitaka Mtaji toka kwa Lowassa na sio MAKAPI
36. Wenyeviti walioletwa na Lowassa ni MZIGO na namjua vizuri. Akithubutu kunijibu ntamwaga UOZO wake wote
37.Nani asiyejua Guninita pia ni mzigo??
38: Nawataka viongozi wangu wanijibu ni mtaji upi walioupata toka kwa Lowassa.
39. Mimi ni Padri Mstaafu, sipendi siasa za uongo.
39.
Ukisema unataka kuiondoa CCM ni lazima ujikumbushe misingi ya
CHADEMA ambayo ilikuwa ni uadilifu. Leo chadema hii ina
Uadilifu gani??
40.
Namshangaa sana Lowassa eti kusimama mbele ya watu akijinasibu
kuwa ni msafi.....kwamba mwenye ushahidi aende Mahakamani. Ni
dhambi kupotosha watu.
41. CCM hawana ujasiri, ni waoga na ndiyo maana wamewalea watu kama akina Lowassa
42.
Ukitoa kinyesi chooni na kukipeleka Chumbani maana yake hata
chumba chako ni CHOO na kitakuwa kinanuka zaidi kulicho choo
cha kawaida
43.Mimi nilikuwepo wakati sakata la Richmond likijadiliwa.Mimi nina ugomvi wa muda mrefu na Lowassa.
44. Mwaka 2010 mimi nilimtaka Lowassa atangaze Richmond ni ya nani.
45.
Leo tena namtaka Lowassa namtaka Lowassa atoke hadharani
atangaze Richmond ni ya nani. Unaposema ni ya mkubwa, atuambie
mkubwa gani
46.
Ukitaka kuijua Richmond rejea Ripoti ya Mwakyembe. Nampongeza
Mwakyembe na Sitta kujitokeza hadharan kuusema ukweli.
47.
Siku moja kabla ya ripoti kusomwa, nililetewa Rushwa ya
milioni 500 ili tukaupindishe ukweli bungeni lakini nilikataa
48.
Ripoti ya mwakyembe iliamua mambo mawili, moja; Lowassa
ajipime au bunge lijadili na lichukue ripoti. Lowassa kuona
hivyo akaamua kukimbilia kujiuzulu kukwepa aibu ya kung'olewa
na bunge
49: Lowassa haaminiki, ni muongo na hastahili kuwa Rais wa nchi....
50. Lowassa ni FISADI na kama mimi ni muongo ajitokeze hadharani akanushe
51. Anasema Lowassa ataleta maji, mbona jimbo lake la Monduli halina Maji???
52.
Mnasema Lowassa kaanzisha shule za kata, iv mjua msingi wa
shule za kata? waandishi rudini shule mkajifunze upya.
53.Nilifanikiwa
kuijenga Chadema na ikawa tumaini jipya la
watanzania.....Vijana wangu wa Chadema, naomba niwe mkweli
propaganda imekivamia chama.
54.
Inasikitisha kuona CHADEMA inajaza mabasi pale jangwani badala
ya watu.....alafu mnawadanganya watu eti ni MAFURIKO
55. CHADEMA ya kipindi changu ilikuwa inakemea Rushwa. Niambien leo chadema watasema nini kwenye majukwaa?
56.
Mnaomtetea Lowassa na nyie jitokezen hadharani...mimi nasema
kwa sababu nina ushahidi na sio lazima ushahidi huu niupeleke
mahakamani.
57.
Wenye uwezo wa kumpeleka Lowassa Mahakamani ni Serikali, na
mwakyembe alisema juzi kuwa kesi ya jinai haina kikomo, mtu
anaweza kushitakiwa muda wowote

0 comments:
Post a Comment