![]() |
"Mimi sikuwa likizo, sikupewa likizo na yeyote. Niliamua kuachana na siasa.. Nilishiriki majadiliano ya kumpokea Lowassa..nikaweka msingi... lakini demokrasia inataka wengi wakiamua unakaa pembeni.."
"CHADEMA Tumaini Jipya lilijengeka nawaambia vijana wangu. Tuache ushabiki. Leo Nina uchungu mkubwa ambayo niliijenga. Kama CHADEMA Leo inasomba watu. Wakati ukifika tutakasikitika tukawa mazezeta siko tayari kuwa zezeta.
Leo tujiulize agenda yetu ni nini?
Katika chama agenda yetu ya kwanza ilikuwa ufisadi Leo iko wapi.
Leo tunageuka na kuwa wabovu zaidi ya Ccm.
Tulikuwa na misingi ya maadili ya Taifa hili.
Kuna mtu aliniambia Dkt. Slaa hujafunga ndoa niliwambia ninyi waandishi serikali ya CCM ndio iliniwekea pingamizi. Ninyi mnamuita mchumba wa Dkt. Slaa mimi namwita mke kwa sababu ndoa hufungwa na Mungu.
Siwezi kupeleka ushahidi mahakamani kwa sababu sina locus ya kesi na wizi ni kosa la jinai hivyo ni ya serikali. Hata wenye kumsafisha Lowassa watoke watueleze."

0 comments:
Post a Comment