Friday, September 4, 2015

Mtangazaji Maimartha Jesse. Mwandishi wetu
Mtangazaji Maimartha Jesse ameibuka na kusema kuwa yeye kama mtangazaji hawezi kushabikia siasa akiamini siyo sahihi kufungamana na upande wowote ingawa kama Mtanzania atampigia kura yule anayeona anafaa. 
Akizungumza na Ijumaa, Maimartha alisema kuwa anawashangaa mastaa kugombana kutokana na siasa na kuweka hadharani hisia zao wakati kikawaida hawakupaswa ili kutowagawa mashabiki wa kazi zao. 
“Mimi siasa kwangu mwiko kiukweli ila kama Mtanzania nitampigia kura ninayeona anafaa kuwa rais wangu, kazi yangu hainiruhusu kiukweli,” alisema. Maimartha.

0 comments:

Post a Comment