Monday, September 7, 2015


Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Luteni Yusuph Makamba amemtaja Mhe. Edward N. Lowasaa kuwa ni fisadi ambaye hafai kabisa kuongoza nchi. Amesema kuwa alikataliwa tangu 1995 kutokana na kuwa na utajiri mkubwa ambao haijulikani ameupataje. Amejimilikisha maeneo Makubwa ya Ardhi na Ranchi zilizokuwa za Taifa mojawapo akiitaja Ranchi ya MZERU Iliyopo Mkoani Tanga na kuwamilikisha pia rafiki zake. Amempatia dada yake tenda zote za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli hadi penseli. Makamba amesema kama ni uongo Lowassa asimame na kukanusha.

0 comments:

Post a Comment