Ikumbukwe Mhe.Jerry William Silaa,ni kijana msomi wa shahada ya kwanza ya ya Mahesabu na Elektroniki toka chuo kikuu cha Dar es Salaam,pia Shahada ya Uzamili toka ESAMI arusha ya uongozi wa Biashara na sasa ansomea Shahada ya Sheria toka chuo kikuu Huria cha Tanzania,ndiye aliyewahi kuwa diwani akiwa na umri mdogo zaidi Tanzania yaani akiwa na miaka 23 tu..Tangu akiposhinda udiwani kata ya ukonga mwaka 2005 hadi 2010..mwaka 2010 hadi 2015 akashinda kuwa diwani kwa kura nyingi kupitia kata ya Gongolamboto jijini Dar es Salaam na baada ya kata hiyo kutenganishwa na kata ya ukonga...2010 hadi 2015 akashika nafasi ya kuwa Meya mdogo zaidi Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alimteua kuwa mjumbe wa kamati kuu (CC) ya CCM Taifa na Sasa ndiye mgombea ubunge mdogo zaidi Tanzania,akigombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM kupitia jimbo la ukonga...
Kama unajijua wewe ni mwana ukonga na
mpenda maendeleo ya kweli,basi usifanye makosa tarehe 25.10.2015..chaguo
lililo sahihi na wazi ni moja tu,Jerry William Silaa awe mbunge
ukonga...
Masama Blog inaungana na wananchi wote
wa ukonga wenye mapenzi mema na maendeleo yatakayoletwa kumtakia kila la
heri kiongozi asiye na shaka katika utendaji wake Jerry Silaa katika
safari hii yake ya muhimu ya kuwawakilisha wananchi wa ukonga katika
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..


0 comments:
Post a Comment