WAZIRI wa Uchukuzi na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM Taifa,Bw. Samuel Sitta, amemvaa mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA, Edward Lowassa aliyehama CCM, kuhamia upinzani baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.
Alihoji kwa nini Lowassa alalamike alionewa kwenye mchakato huo baada ya jina lake kukatwa Mjini Dodoma wakati kulikuwa na wagombea wengi wenye sifa na waadilifu akiwemo mgombea urais wa CCM, Dkt. John Magufuli ambaye ndiye aliyeonekana anatosha.
Bw. Sitta aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni za Dkt. Magufuli uliofanyika katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mkoaniTabora na kuongeza kuwa, Lowassa hana haja ya kulalamika kwani mwaka 1995, aliingia katika mchakato huo akiwa na Rais Jakaya Kikwete lakini alishindwa kupenya kwa sababu ya kukosa sifa.
"Mimi ni miongoni mwa watu waliomtetea sana Lowassa kwenye kikao cha ndani cha CCM wakati akiwania urais mwaka 1995...Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliniita na kuniambia kwa nini namtetea mtu ambaye hafaikuwa rais, ndipo nikasitisha kumuunga mkono.
"Dkt. Magufuli anatosha kuwa rais wa nchi hii; hivyo naomba mumpe kura nyingi kwa sababu ni mzalendo, mtu hodari na mchakapazi anayezijua kero mbalimbali za Watanzania," alisema.
Bw. Sitta alihoji kuwa; "Mwalimu Nyerere hakusema tumpeleke Ikulu mtu ambaye hafai...UKAWA hakuna utaratibu, unaweza kusilimu leo na ukawa Shekhe au kubatizwa na kuwa Askofu," alisema.
Aliongeza kuwa, UKAWA wameazima mgombea kutoka CCM kwa sababu hawana vigezo kwani hata ukienda sokoni, lazima uchague bidhaa yenye vigezo; lakini Lowassa hakuwa na kigezo, hivyo alipaswa kutulia kama wagombea wengine badala yakuendelea kuwadanganya watu kuwa alionewa.
Dkt. Magufuli ahutubia
Kwa upande wake, Dkt. Magufuli alisema kati ya wagombea wote wanaowania nafasi hiyo, hajaona anayeweza kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli zaidi yake; hivyo aliwaomba wakazi wa Taborawampe kura nyingi ili aweze kuwatumikia. Alisema si kila mabadiliko yanayotajwa na wapinzani yana malengo mazuri kwa Watanzania bali mengine yana malengo ya kuwaingiza kwenye matatizo na kuwafanya waishi maisha magumu zaidi.
"Hatutakiwi kufanya majaribio katika kutawala, mabadiliko yoyote hayawezi kuwa mazuri, unaweza kufanya mabadiliko ya kutoka katika nyumba na ukahamia chooni, mimi nitajenga Serikali mpya na yenye mabadiliko ya kweli," alisema Dkt. Magufuli.
Aliongeza kuwa, inashangaza kuona baadhi ya watu wanataka madaraka ya haraka na kusahau walikotoka kwa kueneza uongo kuwa CCM kwa miaka 50 haijafanya chochote; lakini Watanzania hawadanganyiki kwani kila kinachofanyika wanakiona, wanajua walikotoka na wanakoenda.
"Hawa wenzetu wamekuwa wakinadi sera za ajabu wakidai nyumba za matembe zitaisha ndani ya siku 48, hizi ni ndoto za mchana, mimi siwezi kuahidi kama wao; bali nitashusha vifaa vya ujenzi ili kila Mtanzania aweze kujenga nyumba, awe na maisha bora," alisema.
Alisema wapo watendaji wachache serikalini ambao wanaifanya Serikali ionekane mbaya na kusema ameomba ridhaa ya kuwa rais akapambane nao na kuziba mianya ya rushwa.
Bulembo amvaa Sumaye
Akihutubia mkutano huo, Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Alhaj Abdallah Bulembo, alisema inashangaza kuona Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye kudai CCM haikufanya chochote wakatiyeye hakufanya chochote alipokuwa serikalini.
"Sumaye analindwa na walinzi wa Serikali, magari anatumia ya Serikali na mshahara analipwa asilimia 80 halafu leo anasema CCM haifai huyuni muongo," alisema Alhaj Bulembo.
Bashe avunja ukimya
Mgombea ubunge Jimbo la Nzega, mkoani humo, Hussein Bashe, jana alivunja ukimya juu ya minong'ono inayoendelea mitaani dhidi yake kuwa yeye ni shabiki wa UKAWA jambo ambalo si kweli bali yeyeni mfuasi wa CCM na rais ajaye ni Dkt. Magufuli.
Alisema yeye si shabiki wa UKAWA, hawezi kumpigia kura mgombea yeyote anayewakilisha umoja huo bali yeye ni muumini mzuri wa CCM na atahakikisha mgombea urais wa chama hicho, Dkt. John Magufulianapata ushindi wa kishindo Oktoba 25, mwaka huu.
Aliongeza kuwa, amekuwa ndani ya UVCCM tangu mdogo, hivyo hakuingia CCM kutokea barabarani na kuongeza kuwa, Watanzaniawatamchagua Dkt. Magufuli kuwa rais wao si kwa sababu ya diniyake bali wanaamini ataleta mabadiliko yenye uhakika.
Akizungumzia mchakato wa kumtafuta mgombea urais wa CCM Mjini Dodoma, alisema baada ya kupatikana Dkt. Magufuli, makundi yote yameisha na kuomba wananchi wampe kura awe mbunge wao.
Bashe apongezwa
Naye Dkt. Magufuli alimpongeza Bw. Bashe akisema ni mvumilivuambapo mwaka 2005 alipita katika kura za maoni jimboni humo lakini jina lake halikurudi na hakuhama chama kama ilivyokwa wengine.
"Bashe ni muungwana, namuahidi tutafanya kazi kwelikweli, kuahidi shida za wananchi wako nitazitatua," alisema Dkt. Magufuli.
PAPARAZI blog

0 comments:
Post a Comment