Musa Mateja na Imelda Mtema
KIMENUKA!
Siku chache baada ya kumwanika mchumba’ke, raia wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo ambaye tayari amemvisha pete ya uchumba, mambo
yamekuwa siyo mambo kwa staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper
Massawe kutokana na mke wa jamaa huyo kuibuka na kumtaka amwachie
mumewe.
Chanzo makini kimelieleza Ijumaa Wikienda kwamba, baada ya
habari na picha za Wolper na Mkongomani huyo kuripotiwa na gazeti ndugu
na hili, Risasi Jumamosi, mke wa ndoa wa mwanaume huyo alijitokeza na
kuvunja ukimya akimtaka mwigizaji huyo aachane na mumewe huyo mara moja
kabla hajamchukulia hatua za kisheria kwa sababu ameingilia ndoa yake.
“Unajua
baada ya ninyi (Global) kuanika picha za Wolper kwenye gazeti na
mitandao mbalimbali ya kijamii akivishwa pete ya uchumba na Mkongomani,
mke wake ameshindwa kuvumilia hivyo amelazimika kumtumia ujumbe Wolper
akimtaka aachane na mume wake kwani kama alikuwa hana taarifa kuanzia
leo (Jumamosi) atambue kwamba huyo mwanaume ni mume halali wa mtu na ana
watoto ndani ya ndoa.
“Yaani mke wa Mkongomani amemjia juu Wolper
akimtaka amwachie mumewe, ajiweke pembeni mara moja na kama alidanganywa
kuwa huyo mwanaume hajaoa, basi atambue kwamba tayari alishafunga naye
pingu za maisha, tena kanisani na tayari ana familia ya watoto wawili,
haoni sababu ya kumnyamazia maana ameumia sana hivyo anamtahadharisha
ili baadaye asije akaanza kulia akisema hajaambiwa,” kilisema chanzo
hicho.
MSIKIE WOLPER
Ili kuweka mzani wa habari hiyo, Ijumaa
Wikienda lilimtafuta Wolper ili kujua kama ameshayapata malalamiko hayo
ambapo alifunguka kuwa, kuna maneno mengi yanazungumzwa juu ya tukio
hilo lakini ukweli wa mambo zaidi anaufahamu yeye na mchumba’ke huyo
hivyo haoni sababu ya kumwambia kila mtu maana mpaka anafikia uamuzi wa
kuvishwa pete tayari walishajadiliana vya kutosha.
“Naweza kusema
kwamba ni moja ya historia katika maisha ya mchumba wangu hivyo hata
nilipoona hizo picha za mkewe hakuna jambo lililonishtusha kwani tayari
alikuwa ameshaniambia juu ya misukosuko aliyoipitia kwenye ndoa yake
huko nyuma.
“Hadi anafikia hatua ya kunivisha pete basi watu
wanatakiwa kujua tu kwamba kila jambo liko sawa na zaidi wao wanatakiwa
kusubiri hadi siku ya ndoa yetu waone kama itafungwa au lah.
“Siku
hizi dunia imekuwa kama kijiji hivyo huwezi kuwazuia watu kuongea jambo,
mchumba wangu ananijua na mimi ninamjua kwa kina, pamoja na kwamba watu
pia wamekuwa wakimletea maneno kuhusu mimi lakini nimemwambia aachane
nao kwani hakuna sababu ya kujibizana nao, kwa sababu kila mtu ana uhuru
wa kutumia kinywa chake jinsi anavyoweza maana ningekuwa sijui
background (maisha ya nyuma) yake kweli baada ya kuona hizo picha za
mkewe na maneno ya watu wanayosema ingeniuma sana.
“Nafikiri watu
wanachotakiwa kujua juu yetu ni kwamba Mungu akishapanga jambo kamwe
binadamu hawezi kulipangua hata iweje na kwa maana hiyo sasa hata
mwanaume akishakupenda ni ngumu kumsikiliza mtu mwingine maana upendo wa
mtu ni moyo na nafsi yake mwenyewe ndiyo inayoweza kumuongoza kwa kila
hali.
“Watu wameshafanya kila juhudi za kutugombanisha lakini sasa
ameshazoea hadi anavichukulia kama burudani tu, hata mimi haya ninayaona
kama matangazo ya biashara hivyo hakuna linaloniumiza kichwa,” alisema
Wolper.
ETI ANA GUNDU?
Kutokana na kitendo hicho wadau mbalimbali
walifika mbali na kudai kwamba mwanadada huyo inawezekana ana gundu
kwani ameshakuwa na wanaume tofauti na wengine kumvisha pete ya uchumnba
na kutambulishana kwa wazazi lakini ikawa ndivyo sivyo.
“Wolper
anatakiwa kujiangalia sana na kumuomba Mungu kwani siyo mara ya kwanza
kuwa na wanaume wa watu, kinachowaponza hawa mastaa wetu wana tamaa sana
ya fedha ambazo huwasababisha kuwa na mtu kwenye uhusiano bila
kumchunguza vizuri,” alisema mdau mmoja mkazi wa Mwenge, Dar.
TUJIKUMBUSHE
TUJIKUMBUSHE
Kwa Wolper, kuvishwa pete ya uchumba siyo mara ya kwanza kwani awali aliwahi kuvishwa na aliyekuwa mpenzi wake. SOURCE GPL
0 comments:
Post a Comment