Tuesday, September 1, 2015

Nimemsikiliza na kumuangalia usoni Dr. Slaa mwanzo mpaka mwisho, moja ya Degree nilizonazo ni ya Criminology & Police Science nilifundishwa ukitaka kujua binadam anasema ukweli au uongo muangalie machoni muda wote anao ongea: MY OPINION:- Ni kwamba Dr. Slaa ni binadam kama wengine wote ana mazuri na mapungufu na kwenye maelezo yake ya leo yanaonekana very clearly kwanza ameisaidia sana CCM kwa sababu amefanikiwa kusema mengi ambayo yanaacha maswali mengi kuliko majibu kuhusu Uongozi wa Sumaye na Lowasa. He was very strong kwenye FACTS za kwa nini Lowasa na Sumaye sio Agents of Revolution kama nilivyowahi kusema huko nyuma. Mapungufu yake ni kwamba ameyumba sana kwenye sababu za kwa nini ametoka Chadema cause sababu alizozitoa hazikuwa very strong especially pale aliposema kwamba alikubali Lowasa aje Chadema kwa masharti ya kujisafisha na atimize ahadi aliyoitoa ya kuja na Mawaziri na Wabunge 50 wa CCM pamoja na Wenyeviti 22 wa CCM. Well, hapa ninasema ndio mapungufu ya maelezo yake yalipo, kama ni mtu mwenye msimamo kama anavyodai basi alitakiwa kumkataa Lowasa period sio kumkubali kwa masharti I mean what if Lowasa angetimiza masharti yake Dr. Slaa ina maana angekuwa msafi? Otherwise, amejitahidi sana kutuamsha Wananchi na mambo mengi ya hovyo yaliyofanyika kwenye process ya Lowasa kuingia Chadema, na maovu mengi ya Lowasa ambayo tulikuwa hatuyajui kwa mfano la Kutaka kupewa Rushwa ya Shillingi Millioni 500 ili aipinge ripoti ya Kamati ya Bunge ya Richmond. All and all binafsi ninakataa Dr. Slaa kujiunga na CCM na ninakataa Dr. Slaa kuendelea kuwashambulia Lowasa na Sumaye, CCM tuna uwezo wa kushinda huu uchaguzi bila msaada wa Dr. Slaa wala mtu yoyote yule ambaye sio CCM na CCM hatuhitaji ujanja ujanja wa kisiasa kushinda huu uchaguzi, ninataka tushinde huu uchaguzi kwa nguvu yetu wenyewe na we have it. Namba haziko upande wa UKAWA nambaz zipo upande wa CCM, kushika dola unahitaji nambaz sio makelele majukwaani CCM we have the numbers kwa mfano tuna Matawi 955,000 Tanzania nzima tukiyatumia haya matawi ipasavyo tunashinda bila tatizo. CCM tuna wanachama ambao wote wakilipia kadi zao tunatakiwa kuwa na wanachama hai MILLIONI 8 ni mtaji wa kutosha kushinda uchaguzi huu kwa sababu pamoja na Wananchi Millioni 24 kujiandikisha kupiga kura mwaka huu kama miaka mingine wapiga kura hawatazidi Millioni 10. Ninarudia tena CCM twende na tunashinda uchaguzi huu asubuhi saa tatu! - Le Mutuz Nation

0 comments:

Post a Comment