![]() |
| Lowassa na Magufuli |
Vyama
vyote vya siasa vimekubali kufanya mdahalo wa wagombea wa Urais kwenye
vyombo vya habari lakini vyama vinavyounda UKAWA vimekataa kushiriki
kwenye midahalo hiyo kwa kutoa sharti moja la kutomshirikisha mgombea
wao na badala yake waende wenyeviti wa vyama.
Utaratibu
wa dunia nzima kwenye midahalo wanahudhuria wagombea na siyo wenye viti
wa vyama... Yaani Rais Kikwete aache majukumu yake ikulu halafu aende
kwenye vyombo vya habari kufanya midahalo wakati kwenye midahalo
wanazungumzia sera za chama husika na sasa aliyebeba sera za CCM ni
Ndugu Magufuli.
Baada
ya kufanya uchunguzi sababu zifuatazo zimebainika kuwa ndiyo vigezo vya
kumfanya mgombea wa UKAWA ndugu Lowassa kususia midahalo hiyo
1.
Afya yake ni dhaifu na haimruhusu kukaa muda mrefu bila kupewa dawa ya
kumuongezea nguvu. kwenye mikutano yake ya kampeni hajawahi kuzungumza
zaidi ya dakika 15, sasa atawezaje kuhudhuria mdahalo akaongea zaidi ya
nusu saa?
2.
Amehusika sana kwenye kashfa nyingi za ubadhilifu wa mali za umma na
hana uwezo wa kukataa ukweli huo, hata alipoulizwa na waandishi wa
habari huko Dodoma alikataa kulijibu hilo swali, na endapo atahudhuria
kwenye mdahalo wowote hilo swali hawezi kuliepuka
3.
Chama chake hakina sera nzuri, anakosa kitu cha kuongea awapo mbele ya
watu kwakua chama chake hakijaandaa ilani nzuri yenye sera za kumkomboa
Mtanzania. Wakati wenzake wanatoa sera za kupunguza gharama za ujenzi
yeye anamwaga sera za kuwatoa jela akina Babu Seya na kubomoa nyumba za
nyasi nchi nzima kwa muda wa siku 100

0 comments:
Post a Comment