BAADHI ya viongozi wa dini na wananchi wamesema shutuma za aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.
Willibrod Slaa kuwa baadhi yao walihongwa na Mgombea Urais wa Ukawa
kupitia Chadema, Edward Lowassa, ni upuuzi mtupu.
Wamemtaka atoe ushahidi wa madai hayo kwa kutaja majina ya viongozi
na kiasi walichohongwa, wakisisitiza kuwa hizo ni siasa za majitaka na
kwamba anaifanyia kazi CCM ili apate njia ya kurudi katika chama hicho.
Rais wa TEC azungumza
Rais wa TEC azungumza
Akizungumzia shutuma hizo, Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa
Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amemtaka Dk.
Slaa kutoa ushahidi wa madai yake kuwa maaskofu wa kanisa hilo
wamehongwa na Edward Lowassa.
Akizungumza na MTANZANIA kwa simu yake ya mkononi, Askofu Niwemugizi
alieleza kushangazwa na tuhuma hizo zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi ya
maaskofu bila uthibitisho.
“Hizo taarifa ndiyo nazisikia kwako, lakini kama kweli amesema hivyo kwa nini hakuweka ushahidi kuanzia majina ya maaskofu hao waliopewa fedha, kiasi na zilikopokelewa. Lakini kwa upande wangu binafsi sijapokea kiasi chochote kutoka kwa mtu yeyote.
“Hizo taarifa ndiyo nazisikia kwako, lakini kama kweli amesema hivyo kwa nini hakuweka ushahidi kuanzia majina ya maaskofu hao waliopewa fedha, kiasi na zilikopokelewa. Lakini kwa upande wangu binafsi sijapokea kiasi chochote kutoka kwa mtu yeyote.
Askofu Niwemugizi alimtaka Dk. Slaa kutoa uthibitisho wa maaskofu wa
kanisa hilo kupokea fedha kutoka kwa Lowassa waweze kutoa uamuzi.
“Lowassa nimewahi kukutana naye nilimwalika kwenye shule yangu ya
seminari kule Biharamulo… shule yenyewe inaitwa Katoke na nilimuweka
wazi sababu za kumwalika na sikupokea kiasi chochote cha fedha kutoka
kwake,”alisema askofu huyona kuongeza:
“Athibitishe hilo aonyeshe kiasi cha fedha na majina ya maaskofu,
mimi sijapata kiasi chochote labda kama nimetupiwa kwenye akaunti yangu
bila mimi kujua lakini nasisitiza atoe ushahidi.”
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekosti, William Mwamalanga alisema kauli za Dk. Slaa zina dalili ya kuleta kisasi fulani.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekosti, William Mwamalanga alisema kauli za Dk. Slaa zina dalili ya kuleta kisasi fulani.
“Angekuja mapema kabla ya taratibu hizi kuanza tungemwelewa lakini
kwa sasa yupo nyuma ya wakati. Kwanza ameonekana amesukumwa afanye
aliyofanya na hilo haliwezi kuwabadilisha Watanzania walioamua kutaka
mabadiliko,”alisema na kuongeza: “Hotuba yake haina mashiko na taifa
halihitaji watu wabinafsi,”alisema Mchungaji Mwamalanga.
Askofu Gwajima azungumza
Naye Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekana
kuwa mshenga wa Edward Lowassa kujiunga na Chama cha Demokrasia na
Maendelea (Chadema) .
Pia amekana kuhusika kuwarubuni kwa fedha maaskofu 30 wa Kanisa
Katoliki ambao wanadaiwa kumuunga mkono Lowassa katika mbio zake za
urais baada ya kuhongwa fedha.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Askofu Gwajima alisema
Dk. Slaa ndiyo risasi ya mwisho iliyokuwa imebakia ndani kati ya bunduki
ya CCM ili kuwaokoa.
Alisema yote yaliyosemwa na Dk. Slaa ni tuhuma za uongo hivyo
wananchi wazipuuze kwa kuwa mwanasiasa huyo anatafuta uungwaji mkono kwa
wananchi aelekee CCM.
“Yaani ni uongo kabisa tena uongo mweupe, imedhihirisha wazi kuwa
huyu mtu asingefaa kuwa rais. Ni dhahiri ameona akiwasema wanasiasa
wenzake watamjibu kwenye majukwaa yao ya siasa, lakini sasa amewasema
maaskofu kwa kuwa wao hawana majukwaa.
“Kwa hiyo namshauri hayo mambo ya kuwahusisha maaskofu na uchaguzi
aache uongo wa namna hiyo. Nafikiri awaseme wanasiasa wenzake
kuzungumzia mambo ya siasa ila kuwahusisha maaskofu si mambo ya busara,”
alisema.
Akizungumzia suala la kuwa mshenga wa Lowassa na Chadema, Askofu huyo
alisema anafikiri Dk. Slaa ametumwa na waliomtuma, hivyo anawafanyia
kazi watu.
“Kwa kawaida inashangaza kwamba kama watu wawili wanagombana,
inatakiwa awepo mtu wa kuwaunganisha, ila anaposema maaskofu 34 haileti
maana, haiingii akilini… ameingiza Gwajima, Rostam (Aziz) na maaskofu,
haeleweki anachozungumza. Lakini ninachosema kuna waliomtuma ni watu
ambao anawafanyia kazi.
“Kikubwa ni kwamba baada ya Lowasaa kuchaguliwa kugombea urais kwa
Chadema alichukia, alifikiri Lowassa hataendelea kuwa na umaarufu, sasa
anaona Lowassa anakwenda, hiyo imemtia hasira anataka kumchafulia
Lowassa, ndiyo maana anaongelea Lowassa Lowassa tu.
“Kwa mfano alisema Lowasa angekuja na wabunge wenyeviti wa CCM, ina
maana angemkubali Lowassa aje nao, sasa angekuja nao asingekuwa fisadi?
Ni swali zuri ila amekwepa kulijibu.
“Nafikiri Dk. Slaa ndiyo risasi ya mwisho iliyobakia ndani ya bunduki
ya CCM. Natoa wito kwa waumini wangu wafahamu kuwa hizi tuhuma ni za
uongo na namsihi huyo daktari asihusishe maaskofu na uongo wake abaki
nao mwenyewe,” alisema Askofu Gwajima.
Maoni ya wananchi
0 comments:
Post a Comment