Saturday, October 3, 2015

Magufuli amnanga Lissu kwao
Amwita mtukanaji na mkwamishaji miradi ya maendeleo
Diana Chilolo amgeuka lowasa asema hana washauri,

DR Magufuli Alisema Lissu hapaswi kuchaguliwa tena kwa sababu ameshindwa kuwasaidia wananchi wa jimbo hilo kupata maendeleo ya kweli kwa kushindwa kusimamia miradi mingi ya jimbo hilo kutokana na misimamo yake iliyochangia kuwaumiza wapigakura wake.
Ninasema wana Ikungi na Watanzania kwa ujumla tunahitaji kujenga nchi kwa kutumia rasilimali zetu ambazo zitamnufaisha kila Mtanzania, ila kwa hapa kwenu mmeteseka kwa sababu ya aina ya mbunge mliyemchagua. Ni bora kukosea jambo lingine au hata kuoa lakini sio kuchagua, kwani haya ndiyo yanawafanya mteseke. Mnachagua mbunge ambaye kazi yake ni kuwatukana mawaziri na hata zinapojadiliwa bajeti wanatoka nje.
“Waziri naye ni binadamu, hana moyo wa chuma wa kuvumilia matusi, je, kwa hali hii anaweza kuleta maendeleo kwenu. Hapana msifanye makosa kwa kuchagua wabunge wa matusi na kutoka nje,” alisema Dk. Magufuli





0 comments:

Post a Comment