Mwanzoni mwa wiki hii kuna taarifa
zilienea katika mitandao ya kijamii kwamba gari la Mgombea ubunge
kupitia chadema Musoma Vicent Nyerere lilikutwa na milipuko wakati
akifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyabisale Kata ya Bweli
Musoma Mjini, leo Kamishina Msaidizi na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara
Philip Alex Kalangi amezungumza na ripota wa millardayo.com kuhusu
ukweli wa taarifa hiyo.
‘Kuna watu
wawili ambao wanafahamika kwa majina ya Goodluck Msuya miaka (42)
Dereva wa Mgombea Ubunge Musoma Mjini pamoja na Salum Blein ambae pia ni
mlinzi wa mgombea Vicent Nyerere wamekamatwa wakiwa na milipuko kumi na
tano aina ya Explogel 7M V6 Watergel explosive’- RPC Philip Kalangi
‘Milipuko
hiyo ilikutwa kwenye gari la Mgombea Ubunge lililokuwa likiendeshwa na
dereva wake kabla ya kukamatwa watu hawa, Mgombea Ubunge Ndugu Vicent
Nyerere alikuwa akiendelea na mkutano ndipo mlinzi wake alikwenda
jukwaani na kumpa taarifa kwamba ndani ya gari lake kuna milipuko,
mgombea huyo wa ubunge aliwambia wavipeleke vitu hivyo jukwaani na ndugu
Nyerere aliwatangazia wananchi kuwa kuna watu wanataka kumuuwa na
wamemtegea bomu ndani ya gari lake’ – RPC Kalangi
‘Katika
uchunguzi wa awali wataalamu wa uchunguzi wamesema kweli ilikuwa ni
milipuko ambayo kwa wakati huo ilikuwa haijafikia wakati ya kuleta
madhara na kutokana na maelezo ya awali dereva na mlinzi wa Mbunge huyo
yalitia shaka na ndipo ilipelekea kukamatwa kwani muda wote wao ndio
walikuwa na gari hilo na hakuna mtu mwingine alilitumia kwa siku hiyo,
kwa sababu sio swala la kawaida tukishagundua kuwa ni mifuko na ukaweza
kubeba na kuurudisha’-RPC Kalangi
‘Kuhusu
kwamba walikuwa wametega bomu la kutaka kuumua Mheshimiwa hilo bado
tunalichunguza kutokana na mazingira ya tukio lenyewe lilivyotokea na
tayari mgombea Ubunge ameshahojiwa ametoa maelezo yake bado tunaendelea
kuhoji watu wengine’-RPC Kalangi
0 comments:
Post a Comment