Posted by Williammalecela.com on Monday, October 19, 2015
Rais Kikwete afanya uteuzi katika Mahakama nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi katika Mahakama kama ifuatavyo;
Rais amemteua Bi. Katarina Revocati kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania (Chief Registrar). Kabla ya uteuzi huu, Bi. Revocati alikuwa
Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Rais pia amemteua Ndugu John Rugalema Kahyoza kuwa Msajili wa
Mahakama ya Rufani na kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kahyoza alikuwa Msajili
wa Mahakama Kuu.
Mwingine aliyeteuliwa ni Ndugu Ilvin Claud Mugeta ambaye anakuwa
Msajili wa Mahakama Kuu. Kabla ya Uteuzi huu ndugu Mugeta alikua
Mkurugenzi wa Ukaguzi na Maadili.
Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Oktoba,2015.
MWISHO
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
19 Oktoba, 2015
0 comments:
Post a Comment