MCHUNGAJI wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima aliyejipapambunua kuunga mkono mabadiliko asiyoyajua ya UKAWA, kabla
haujafanyika uchaguzi mkuu Jumapili, mwishoni mwa wiki hii miongoni mwa
propaganda zao zimeanza kuthihiri uongo.
Watu hawa ambao moja kati ya ahadi zao ni kuwaleta
binadamu wenzetu waliotangulia mbele ya haki hadharani wakati familia zao
wanaamini wamekufa, wiki hii ni walikuwa miongoni kwenye mazishi ya aliyekuwa
mwenyekiti mwenza wa UKAWA, Bw. Emmanuel Makaidi.
Kwa nini?
Kama wangekuwa na uwezo wa ufufuo, wangeanza na
kiongozi wa nafasi nyeti katika umoja, lakini wameshindwa na jambo hili ni wazi
ni kuwa ni majaribu ya mwenyezi Mungu, tukiomba Watanzania watupishilie mbali
na aina hii ya uongozi.
Dura za kisiasa zikionyesha CCM kushinda kwa
kishindo na kustaajibisha watu, hiyo kutokana na mgombea wake ambaye yupo
jijini Dar Es Salaam kwa siku tatu huku jijini Mwanza ambayo ndiyo ngome kuu ya
kura za Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
kutokana na idadi yake ya watu, UKAWA wamekuwa wakijiaminisha tu bila takwimu
zozote watashindaje.
Leo katika habari hii, tutamalizia pia sehemu ya
pili ya Edward Lowassa na mchungaji Gwajima, kwa vile sitakuwa na muda tena wa
kuwazungumzia baada ya Jumapili, Lowassa kurejea Monduli moja kwa moja.
Atarejea kwa sababu ndani ya CHADEMA hana cheo
chochote na si mtendaji wa aina yeyote wa shughuli za kila siku, hivyo hatakuwa
na sababu tena za kwenda ofisi za CHADEMA alizoingia kwa siku moja tu, hadi leo
hana sababu ya kuingia tena ofisi hizo.
Hiyo pia itakuwa kwa Mzee wangu Kingunge Ngombale
Mwiru, Khamis Mgeja, Makongoro Mahanga, Lembeli na Ester Bulaya ambao watabaki
kutumiwa posho tu na Lowassa kama shukrani za kumuunga mkono lakini CHADEMA
haina kazi nao tena, natanguliza pole zangu nyingi kwenu.
Leo nikiamini Gwajima aliijua mipango ya upinzani
muda mrefu kiasi alipata jeuri ya kumkutana Kardinal Polycap Pengo,
iliyomfikisha kwenye matatizo aliyonayo mahakamani kwa sasa.
KIVIPI ? Edward Lowassa ambaye katika mikutano yake
ya kampeni ameshindwa kuwaeleza Watanzania aina ya mabadiliko atakayoyaleta na
jinsi gani atauondoa umaskini anaoupigia jaramba, ni maigizo kama yalivyokuwa
kwa Josephat Gwajima alipokamatwa na polisi kuigiza anaumwa na kulazwa TMJ ili
kupata huruma za waumini wake.
Marafiki hawa wanaoshabihiana kwa uigizaji na pia matamshi
yao kama nilivyobainisha sehemu ya kwanza, sasa kwa wenye akili timamu
tunagundua kwa nini Askofu Gwajima alipata jeuri ya kumtukana Askofu Polycap
Pengo. Ana kesi mahakamani ya kujibu, hivyo Lowassa anaposema
imefikia wakati sasa Walutheri kutoa Rais, maana yake kesi ya Gwajima
itakwisha. Na itakwisha kwani Lowassa akiwa ameshatangaza kuwatoa jela akina
Nguza Viking na mwanae Pappii Kocha, kivipi asiweze kuiondoa mahakamani kesi ya
Gwajima kumtukana Pengo.
Kwa mantiki hiyo kujiaminisha kwao hadi alitukana ni
kwamba si lazima wapate kura za dhehebu la
Roman Catholic ambako Askofu wao Pengo alishaambiwa “ Amekula maharage
eeh…aah mpuuzi mmoja… mjinga mmoja, asiyefaa mmoja !.
Kwa, wanaoongozwa na Kardinal Pengo lazima
wajitafakari inakuwaje aliyemtukana kiongozi wao, sasa anapanda jukwaani
na Lowassa wakiitaka nchi kwa
kuzungumzia dhehebu moja tu kati ya Wakristo lukuki. Kama ubaguzi kwa Wakristo
wenyewe kwa wenyewe umefikia hapo, vipi kwa Waislam?
Maigizo haya yatatupeleka tusikotarajiwa, Watanzania
kweli tunataka nchi ibadilike iende na wakati kutokana na Dunia inavyokimbia
kwa sasa, lakini mabadiliko yanaanza kwetu wenyewe, tusome na kupata uelewa
mkubwa wa mambo ya Dunia na kukimbizana na soko la ajira, pia tufanye kazi kwa
bidii.
Si kweli, Machinga anayeuza maji Kariakoo akiingia
Lowassa madarakani mwaka huo huo, maisha yake yanakuwa tambalale. HAIWEZEKANI
ASUBUHI UUZE JUISI KWENYE NDOO YA MAJI JIONI UKAKAE KITI KIREFU UNAKUNYWA BIA,
UTAENDELEA KWA MTAJI UPI ?
Wapo walioendelea kwa kujisomesha na wapo
walioendelea kwa kuuza juisi kwenye ndoo ya maji hatimaye wakapata vioski
vikubwa vya kuunza vinywaji baridi hadi kufikia kujenga nyumba. Wamefanya kazi
na kujiwekea malengo, hivyo kufanya kazi kwa bidii ni mabadiliko tosha ya
maisha yako ya sasa ulipofikia.
Tunahitaji mabadiliko, halafu nini kinafuata ama
kitafuata tu baada ya mabadiliko ? Nchi haisimami, dunia inasonga mbele
tutasimama wakigombea madaraka kwenye mabaraza ya mawaziri, wakimaliza
watagombea ukuu wa mikoa, wilaya na makatibu wakuu hiyo ni miezi mitatu kama si
sita.
Narudia tena genge lililomzunguka Lowassa kutaka kuingia
IKULU la Gwajima na wengineo ni tatizo ambalo heri mara 100 ya CCM mzee. Ndio
maana CHADEMA badala ya kumfanyia kampeni Lowassa kwa wakati huu wanapambana kumsafisha,
huku wasishaji wenyewe wakiwa wachafu mikononi, usoni na mioyoni mwao.
OMBI langu kwa Watanzania walioweka nadhiri ya kukaa
vituoni kulinda kura kama kweli wanafikiri wataibiwa na wanaamini hivyo,
wafuate ushauri huu;
CHA
KUFANYA; UKISHA PIGA KURA ILI UILINDE
VIZURI KURA YAKO USIKUBALI KUIDUMBUKIZA KWENYE KISANDUKU, BAKI NAYO ILI
USIIBIWE UKIWEZA MPELEKEE MHUSIKA ALIYEKUSHAWISHI UBAKI KUILINDA ILI UMWONYESHA
UNAYO HAIJAIBIWA.
Tutafakari sana kila tunalolilisikia tulipime sana,
Mtanzania tusikurupuke, nchi ipo mikononi mwako. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu
Ibariki Afrika.
Le Mutuz Nation
Le Mutuz Nation

0 comments:
Post a Comment