Msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha
BAADA ya kula bata kwa mwezi mmoja huko Dubai
anakodaiwa kuwa pamoja na mfanyabiashara tajiri wa mafuta,msanii wa
muziki na filamu Bongo, Baby Madaha amerejea kwa mbwembwe, akisema
anajiandaa kufungua kampuni.
Msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha
Akizungumza na gazeti hili, Baby Madaha alisema anatarajia kufanya
uzinduzi wa kampuni hiyo ambayo pamoja na mambo mengine, itashughulika
na filamu.
“Hapa ninapozungumza na wewe nipo bandarini nachukua vifaa
nilivyonunuliwa na mpenzi wangu huko Dubai na baada ya zoezi hili
nitarudi huko kwani ndipo yatakuwa makazi yangu makubwa,” alisema Baby
Madaha.

0 comments:
Post a Comment