Wednesday, November 4, 2015

Linah Sanga amekanusha uvumi kuwa ana ujauzito na kuweka taarifa sawa
 kuhusu afya yake ya uzazi
 Mwimbaji huyo wa ‘No Stress’ amesema 
kuwa kwasasa anajipanga ndio maana hajaamua kupata mtoto lakini 
hiyo haimaanishi kuwa ana matatizo yoyote ya uzazi kama badhi ya watu 
wanavyohisi
 Mimi nipo vizuri bhanaa sina tatizo la uzazi ila huwa najipanga ndio maana watu hawajahi
 kuniona nina ujauzito, lakini kwa sasa najiachia sanaa hivyo
 muda wowote wanaweza kusikia jambo  
alisema Linah kupitia Planet Bongo ya EATV, 
Hii si mara ya kwanza Linah kukanusha taarifa za kuwa mjamzito. 
Mwaka jana (2014) mwanzoni Linah aliwahi kukanusha taarifa kama hizo, na kusema
  maswala ya ujauzito, kuolewa na kuwa na familia ni ya muhimu kwa kila msichana
 lakini upande wake muda wa kuvifanya hivyo ulikuwa bado.

0 comments:

Post a Comment