Tuesday, November 3, 2015

Barnaba afanya kazi na msanii mwingine wa Uganda, Kleyahâ
  Wawili hao wanarekodi wimbo uitwao Msobe Msobe

 katika studio za High Table zinazomilikiwa na Barnaba. ,Kleyah alinitafuta kupitia simu alipewa namba yangu kupitia kituo kimoja hivi cha redio. Ni msanii ambaye mwenye uwezo mkubwa sana na sikutegemea kama msanii kama huyu anaweza kunitafuta maana nilimfutilia nikaangalia biography yake ipo vizuri, lakini aliniamini na ndio maana tukafanya kazi. Nimemuimbisha Kiswahili humo ndani vizuri ameimba. Kleyah ni msanii aliyezaliwa nchini Uganda na kuchukua elimu yake ya juu katika masuala ya mawasiliano katika chuo cha Phoenix nchini Marekani. Kwa sasa Kleyah anaishi nchini Tanzania akiwa anatarajia kukamilisha masomo yake ya utawala wa kimataifa (Degree in International Management).

0 comments:

Post a Comment