Tuesday, November 3, 2015

Staa wa Pop nchini Marekani, Taylor Swift anashtakiwa kwa kuiba mashairi ya wimbo wake wa mwaka 2014, Shake It Off na anatakiwa alipe dola milioni 42.

Muimbaji wa R&;B, Jesse Braham, 50, anadai kuwa Swift aliiba maneno kutoka kwenye wimbo alioundika mwaka 2013 uitwao  Haters Gone Hate.

Pamoja na kutaka alipwe kiasi hicho cha fedha kama fidia, Braham anataka jina lake liongezwe kama mwandishi wa wimbo huo. Wawakilishi wa Swift bado hawajajibu chochote kuhusiana na kesi hiyo.
Braham anasema ana umiliki wa kisheria wa maneno ‘haters gone hate’ na ‘playas gone play’ yaliyotumika kwenye chorus ya wimbo wa Swift.

Kwenye chorus ya Braham’ maneno yaliyopo ni: “Haters gone hater, playas gone play/ Watch out for them fakers, they’ll fake you everyday.”

Chorus kwenye  Shake It Off ya Swift inasema: “Cause the players gonna play, play, play, play, play/ And the haters gonna hate, hate, hate, hate, hate. And the fakers gonna fake, fake, fake, fake, fake.”
Hata hivyo nyimbo hizo mbili hazifanani zinavyoimbwa.

Braham, ameiambia New York Daily News kuwa anaamini kuwa hakuna jinsi Swift anaweza akawa ameandika wimbo huo mwenyewe. “Her hook is the same hook as mine. If I didn’t write the song Haters Gone Hate, there wouldn’t be a song called Shake It Off,” alisema.

Amesema tayari ameshazungumza na lebo ya msanii huyo, Big Machine kwa zaidi ya mara nne kuhusu suala hilo. Awali alitaka jina lake liandikwe kama mwandishi wa wimbo huo na pia aliomba apige ‘selfie’ na mrembo huyo lakini alitoswa kwa kuambiwa kuwa madai yake sio halali.

“At first I was going to let it go, but this song is my song all the way,” alisisitiza.

0 comments:

Post a Comment