Monday, November 23, 2015

CLIPPERS

Toronto  Raptors walikuwa na kazi moja tu alfajiri ya leo nayo ni kuzima makali ya Blake Griffin na Chris Paul, na kisha ilikuwa inatosha kusifumulia  mbali Los Angeles Clippers
.

Demar DeRozan alikuwa na pointi 21, DeMarre Carroll alifunga kila ya pointi zake 21 katika kipindi cha kwanza, na Raptors ikawafanya  Griffin na Paul  kucheza zaidi ya dakika  20 bila kufunga pointi yoyote na kupata ushindi wa  91-80 dhidi ya Clippers.

” Tunawaheshimu sana Griffin na Paul kwa sababu wao ni All-Stars , lakini siyo mara ya kwanza tumekuwa tukicheza nao,” centre  Bismack Biyombo alisema baada ya kufpata kuanza kwenye  mechi yake ya kwanza ya msimu kuchukua nafasi ya majeruhi Jonas Valanciunas .

“Leo hii walinzi wetu na Bigs wetu walifanya kazi nzuri ya kuwapeleka na kuwatoa kabisa  kwenye  mchezo . Tulifanikiwa kuanza  mchezo kwa  njia sahihi, na ilitusaidia sana kupata hiki tulichokipata. ”

Luis Scola aliongeza pointi 20 na Kyle Lowry alikuwa na pointi 13 na pasi 10 kwa Raptors ( 9-6 ). J.J.

Redick alifunga pointi 17 kwa Los Angeles (6-7) , ambayo imepoteza michezo  mitatu mfululizo  na saba kati ya  tisa baada ya kuanza msimu 4-0.

0 comments:

Post a Comment