Lillard alikuwa na pointi 30 huku akitoa pasi zake nyinngi zaidi kuwahi kupata 13 , na CJ McCollum aliongeza pointi 19 katika ushindi wa Blazers ambao ni wa sita mfululizo dhidi Los Angeles Lakers, na kuibuka na ushindi wa 107-93.
Mason Plumlee aliongeza pointi 17 na 11 rebounds kwa Blazers , ambao walishinda mchezo wao wa pili mfululizo baada ya kupoteza takribani michezo saba.
Mchezaji Jordan Clarkson ameendelea kuwa mchezaji ambaye ndio yupo vizuri kwa sasa kwa klabu ya Lkaers akiiongoza klabu yake katika mchezo huo kwa pointi 19. Kobe Bryant alifunga pointi 18 akipata mitupo 6 pekee kati ya 22 aliyojaribu huku pia akikosa mitupo yote mitano ya pointi 3.
Lakers sasa wamepoteza michezo itatu mfululizo huku pia rekodi yao ya sasa 2-11 ikiwa ni mchezo mmoja pungufu kufikia rekodi ya kuanza msimu vibaya waliyoweka msimu uliopita ambao ulikuwa ndio msimu mbovu zaidi katika rekodi ya klabu hiyo.
Kitendo cha Bryant kushindwa kupata mtupo wowote wa pointi 3 katika mitano aliyojaribu inamfanya kuwa amepata mtupo mmoja tu kati ya 14 aliyojaribu ya pointi 3 katika michezo 3 ya mwisho. Lakini pia amekuwa na rekodi mbovu ya kupata mitupo 14 tu kati ya 70 aliyojaribu ya pointi 3 msimu huu.
0 comments:
Post a Comment