Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Kila kitu ukizidisha ni sumu! Ndivyo ilivyotokea kwa staa wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye anadaiwa kumtupia lawama
mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuwa amemharibu
mtoto wao, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ kwa kumzidishia vikorombwezo
vya urembo, Ijumaa Wikienda limetonywa.
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.
Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika ambacho ni ‘memba’ wa familia
ya Diamond au Dangote au Chibu zilieleza kwamba, kitendo cha Zari
kumpodoa Tiffah kupita kiasi kimekuwa kikimpa shaka jamaa huyo akihofia
kuwa kinaweza kumsababishia mwanaye kilema.
“Unajua mwanzoni Zari alianza kwa kumpaka lipstick na kumchora wanja
lakini Diamond hakuona ni ishu sana.“Lakini Zari alipoanza kumwekea
mawigi na kope za bandia, ndiyo jamaa akashtuka na kuanza kuuliza kama
zina madhara au hazina?
“Kila Zari akitupia picha za Tiffah kwenye mitandao ya kijamii kama
Instagram zikimuonesha akiwa na mawigi na kope bandia ndivyo maoni ya
watu yanazidi kuwa mengi wakimponda kuwa anamharibu mtoto wa Diamond.
“Daktari alimweleza kope bandia huongeza uzito kwenye misuli ya kope
halisi, matokeo yake huifanya misuli ilegee na kuna uwezekano wa
mbandikaji au mbandikwaji akawa kipofu japokuwa madhara hayo hayawezi
kuonekana ndani ya muda mfupi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
Kufuatia ishu hiyo, Diamond amekiri kuwasiliana na Zari ambaye
amemtoa hofu kwamba ni mambo ya kutengeneza kwenye kompyuta siyo
vikorombwezo vya kweli.


0 comments:
Post a Comment