Posted by Williammalecela.com on Wednesday, November 18, 2015
Exclusive: Haya ndio mambo ambayo Alikiba anahisi kufanyiwa ili asifanikiwe
Bongo5
imemtafuta mtu wa karibu kwenye uongozi wa Alikiba kutaka kujua kile
ambacho wanahisi msanii wao anafanyiwa na wengi hawavijui.
Mtu huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alidai kuwa kuna watu ambao
wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kuhakikisha kuwa Alikiba hafanikiwi
kimataifa.
Ametolea mfano video za Mwana na Chekecha Cheketua pamoja na kuwa na
viwango vinavyokubalika na kuongozwa na waongozaji mahiri barani Afrika,
kituo cha MTV Base hakijawahi kuzicheza na wanapokuwa wakiuliza sababu
wameshindwa kupewa maelezo yasioeleweka.
Tunawatumia MTV Base, video wanazipokea na wanatuma confirmation ya
kuzipitisha lakini hatuelewi kwanini hawazichezi tena, amesema.
Amedai kuwa waliwapa Soundcity kipaumbele cha kucheza video ya Mwana kwa
mara ya kwanza lakini baada ya hapo video hiyo haikuwahi kuchezwa tena.
Hata zile Top Ten East yao haikustahili kuingia kweli? Kuna video ngapi
za Afrika Mashariki zinaingia kwenye top ten na zingine ni za kawaida tu
iweje Mwana isichezwe? amehoji.
Kinachoshangaza zaidi, kuna watu wanawaambiaga wasanii ukitaka kutoboa tobo kimataifa lazima upitie kwao.
Kwa mifano hiyo amedai kuwa Alikiba anahisi kuna watu wanaofanya kila
njia hata kwa kumwaga fedha ili kuhakikisha kuwa jitihada anazozifanya
hazifiki popote na kwamba kitu hicho kinamnyong'onyeza sana.
Ametoa mfano jinsi ambavyo Alikiba anakubalika nchini Kenya anakopachukulia kama nyumbani pia.
Ametolea mfano wimbo wa Nagharamia alioshirikishwa na Christian Bella
kuchezwa kwa zaidi ya mara 10 kwenye kipindi cha Classic 105 Maina In
The Morning kinachoendeshwa na Maina Kageni aliyewaambia kuwa hakijawahi
kutokea kitu kama hicho kwenye historia ya show hiyo.
Kuhusu tuzo, amesema uongozi pamoja na Alikiba mwenyewe wameamua sasa
kutojihusisha na na baadhi ya tuzo wanazohisi zina mrengo wa kibiashara
zaidi.
Ali ameamua kuweka focus yake zaidi kwenye muziki wake na mashabiki na sio tuzo, amesema.
Hafanyi muziki ili apate tuzo anafanya muziki kwa ajili ya mashabiki
zake. Tuzo zitakuja tu by the way lakini sio his main focus. Why Tuzo
nyingi duniani siku hizi zinaanzishwa au zinaendeshwa kibiashara zaidi.
Ni tuzo chache ambazo zimebaki kwenye misingi na zina credibility ya
kueleweka. Kwa mfano tuzo zile Afrimma za US walimuweka kwenye kipengele
cha upcoming, Ali ni legend. So unaweza kuona kabisa kwamba hawafutilii
wanaweka tu watu ili tuzo zao zipate kiki, amesisitiza.
So alichoamua yeye baada ya kuzungumza na management kwamba from now on
hatojihusisha kabisa na awards ambazo hazina credibility,ambazo
zimeanzishwa au zipo kwa ajili ya kutumia wasanii kibiashara au kwa
manufaa binafsi ya waandaji na sio kuwatuza kutokana na ubora wa kazi
zao.
Ali atashiriki kwenye awards lakini zile ambazo zina mrengo wa kuwatuza
wasanii kwa ubora wa kazi na sio zenye mlengo wa kuwatumia kibiashara na
mwishowe zinatengeneza vita/uhusiano mbaya baina ya wasanii.
Mfano mwingine ni hii Afrima ya Nigeria walimuweka kwenye categories
ambazo hakustahili kama Album of the year, Ali hajatoa albam since 2009!
Hizi zote zinaonyesha hawana umakini na wanafanya tu vitu kwa
kukurupuka bila ufuatiliaji mzuri, hence no credibility.
Pamoja na yote hayo Alikiba anadai anapenda watu wafahamu kuwa yeye si
mtu mwenye kinyongo na mafanikio ya wasanii wengine na kwenye mahojiano
na Diva aliwapongeza Diamond na Vanessa Mdee kwa ushindi wao.
Wengi hawanijui tabia yangu lakini wanahisi labda mimi nina wivu ama
nini. Hapana mimi nasupport muziki na nampenda kila mtu,alisema Kiba.
Chanzo: bongo5
0 comments:
Post a Comment