Watu wametishwa. Watu wametishika. Makada watakosa za watoto ada.
Kujenga kutasimama. Miradi itapigwa radi na kuishia kuwa ahadi. Chama
kina utawala wake. Chama kina Mwenyekiti wake. Si huyo Rais wa Tanzania.
Kwanini majipu ya chamani nayo yapaniwe kutumbuliwa?
Tumepata taarifa, isiyo na ya kuvutia sifa,kuwa jamaa anataka kupewa
nafasi ajinafasi kuyatumbua majipu ya chamani. Lakini, ameombwa asubiri
wakati wake ufike. Makada wanakipenda chama kwa 'maslahi yanayoleta
uhai'. Yakikaushwa ghafla,hapatatosha. Lakini, Ofisi Ndogo za CCM
Lumumba hapakaliki. Hakuna raha ila karaha kusubiri pigo la ghafla.
Makada nchi nzima wanamuunga mkono Rais kutumbua majipu pengine lakini
si chamani. Chamani kunafukuta kwa hofu ya 'bifu' kuporwa mnofu. Makada
wanatumikia chama na wao wenyewe. Wanatamani wale waminywe na wao
wasiguswe ili wasisuse. Hawataki sera ile ifike humu chamani.
Serikalini sawa, chamani si sawa. Double standards!
0 comments:
Post a Comment