Wanasayansi wa Ulaya wameanzisha utafiti rasmi kuamua iwapo kuwalisha ngurue na kuku wadudu ni salama kwa afya zao na walaji.
Kulingana
na utafiti unaoungwa mkono na shirika la Ulaya la Usalama wa Chakula,
funza waliokaushwa au nzi wa kawaida wa nyumbani wanakaushwa na kusagwa
kabla ya kuchanganywa na nafaka inayotumiwa kulisha ngurue na kuku.
Matumizi
ya protini katika utengenezaji wa vyakula vya mifugo yamepigwa marufuku
tangu kuzuka kwa maradhi ya kichaa cha ng'ombe miaka ya 80.
Hatua hii imeleta upungufu mkubwa wa protini katika chakula cha mifugo.
Inaaminika kuwa wadudu wana kiwango cha juu zaidi cha protini hadi asilimia 60.
Mradi
huo unataka kuthibitisha iwapo mifugo hao wanaweza kula vyakula
vilivyochanganywa na wadudu hao kwa njia ambayo watanufaika bila
kusababisha maafa kwa watumizi wa bidhaa ya mifugo au kuku hao.
Wanasayansi wanasema kuwa iwapo mpango huo utafaulu, chakula hicho kinaweza kuwa mbadala wa maharagwe ya soya.
0 comments:
Post a Comment