Baada ya kipindi cha kampeni kupita Kala Jeremiah pia yuko kwenye foleni ya wasanii wanaotaka kutoa kazi mpya za kufungua mwaka.
Kala amesema kuwa tayari video ya kazi mpya imekamilika na anatarajia kuitoa hivi karibuni.
“Video ya wimbo mpya na nimeshoot na PABLO ila nisingependa kwanza kutaja jina la wimbo, lakini mwezi wa 12 lazima itoke”.
Video nne zilizopita za Kala (Nchi ya Ahadi, Usikate Tamaa, Simu Ya Mwisho, Wale Wale) zote zimeongozwa na Pablo, kuhusu kwanini ameamua kumtumia director mmoja kwenye video zake nyingi Kala amesema;
“Pablo ni director ambaye anakubali mawazo ya msanii ukizingatia mimi huwa naandika mwenyewe script ya video zangu. Siyo kila director ataheshimu mawazo ya msanii na mimi pia huwa siamini mawazo ya director maana mimi ninapouandika wimbo naiona na video yake itakuwaje. Napenda kufanya kazi na pablo maana anaheshimu mawazo yangu na huwa anasaidia kuongezea mawazo na siyo kufanya kila kitu yeye. Pia kila nikifanya nae huwa tunapata video nzuri sana” alimaliza Kala.
0 comments:
Post a Comment