Monday, November 16, 2015


1 hr · Edited · 
Ole Mushi
Pichani ni Mwanajeshi Mkakamavu wa zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Arusha Mjini, Waziri wa Zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Katibu Mkuu Mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akionekana Mtanashati katika Vazi lake la Uspika wa Bunge la Afrika Mashariki.
Picha hii ilipigwa wakati Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kuwa Spika wa Kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki, nafasi ambayo aliishika kwa Muda wa Miaka mitano
Kinana pia anatajwa kuwa Meneja wa Kampeni wa CCM katika Uchaguzi wa Mwaka 1995 uliomuingiza Madarakani Rais Benjamin William Mkapa na pia Mwaka 2005 na 2010 katika Uchaguzi Mkuu uliomuingiza Madarakani Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Kinana pia ameshiriki kama mwenyekiti wa kamati iliyomwingiza madarakani Mh Magufuli 2015.
Kabla ya hapo kama katibu Mkuu wa chama aliweza kuzunguka Tanzania nzima akisikiliza kero za wananchi na kuisimamia serikali. Mpango huo umeonekana kukiimariasha zaidi chama cha mapinduzi na kukisogeza karibu zaidi na wananchi.
Kinana ni mtu mwenye msimamo sana japokuwa huonekana mtulivu hasa wakati wa kuongea. 
Yeye ndiye muasisi wa dhana ya mawaziri mzigo na amekuwa akitoa msukumo mkubwa sana kwa serikali kuwashughulikia mawaziri na watendaji wazembe. 
Kama mtendaji Mkuu wa chama ndiye katibu Mkuu aliyekiongoza chama katika kipindi cha upinzani mkubwa. Si siri kampeni za mwaka 2015 zilikuwa za kipekee ila kakivusha chama.
Anaelewana zaidi na vijana ndio maana katika kipindi chake cha Uongozi vijana wengi wamepewa nafasi na chama. 
Ni mjenzi mzuri wa hoja kutokana na utulivu wake anavutia zaidi kumsikiliza. Hapendi siasa za kushambulia ni mtu anayesoma mchezo kabla ya kujibu hoja. 


Anapinga swala la waziri Mkuu kuwa mwenyekiti wa wabunge wa chama cha mapinduzi. Pia aliwahi kuwakemea wabunge wa Ccm KUKUBALI kila kitu Bungeni.


Neno moja kwa fundi huyu aliyesimama Nyuma ya mafanikio ya CCM.


Thadei Ole Mushi.

0 comments:

Post a Comment