Ofisa msaidizi wa Programu kutoka Forum CC Jonathan Sawaya akizungumzia kuhusu mkutano mkubwa wa mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika Ufaransa.
Evelina Mageni ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 akizungumza umuhimu wa wakulima kushirikishwa katika kutunga sera, utunzaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo.
Kushoto aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Edna Kiogwe akichangia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari kuelekea mkutano mkuu wa Tabia nchi.
1
TAMKO LA ASASI ZA KIRAIA KUHUSU MKUTANO WA ISHIRINI NAMOJA WA MABADILIKO YA TABIANCHIKuanzia mwishoni mwa mwezi Novemba hadi katikati ya mweziDisemba, Mataifa wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchichini ya Umoja wa Mataifa (UNFCCC) yanakutana jijini Paris-Ufaransakatika mkutano wa ishirini na moja wa wanachama (COP21). Mkutanohuu unalenga kwa mataifa wanachama kukubaliana mkataba mpya wamabadiliko ya tabianchi ambao unalenga kupunguza uzalishaji wa gesi joto na pia kutengeneza namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.Kuelekea katika mkutano huo; mashirika ya ForumCC, NorwegianChurch Aid Tanzania na Oxfam Tanzania, kwa pamoja tumeandaa jumuiko la kutathmini mahitaji ya Watanzania kwenye mkutano huo.Jumuiko hili litafanyika siku ya
Ijumaa, tarehe 20 Novemba 2015,katika viwanja vya kijiji cha Makumbusho kuanzia saa 2:30asubuhi hadi saa 9:30 mchana
.Malengo ya jumuiko hili ni:
Kutathmini mahitaji ya wananchi kwenye mkutano wa COP21;
Kupaza sauti kuhusu maeneo makuu ya kuwekeza kwa wakulina wadogo wadogo;
Kuwakutanisha wadau mbali mbali kwenye sekta ya uzalishajichakula na mabadiliko ya tabianchi; na
Kusherehekea na kuongeza nguvu za pamoja katika jitihada zakukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
![]() ![]() ![]() ![]() ![]()
Kunauhusiano mkubwa kati ya mabadiliko ya tabianchi na uzalishaji wachakula. Wanawake wazalishaji chakula wadogo wadogo wanazalisha70% ya chakula hivyo wao ndio waathirika wakuu wa mabadiliko yatabianchi. Pamoja na kuathirika huku bado wamekuwa wazalishajichakula wakuu katika Taifa letu. Licha ya juhudi za wakina mama hao bado mchango wao haujatambulika na kupewa kipaumbele kwa kiwangokikubwa.Mazingira, hali ya hewa na uzalishaji chakula ni mambo yanayokwendapamoja. Uwepo wa hali nzuri katika mambo haya matatu ni mafanikiomazuri ya uzalishaji chakula. Dunia inapaswa kuchukua hatua muhimuza kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kwani ni dhahiri kuwa duniainaweza kupoteza uhalisia wake, na hivyo kuathiri maisha ya binadamuna viumbe wengine ukiwemo uzalishaji chakula. Katika kusanyiko hili wazalishaji chakula kutoka mikoa mbalimbali Tanzania watakusanyikana kuongelea juu ya changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na jinsi yakukabiliana nazoKusanyiko hili ni sehemu muhimu ya kuwapa nafasi wazalishaji chakula wadogo wadogo kutoa maoni yao. Wanawake wazalishaji chakula watapata nafasi ya kongea kuhusu faida ya kazi zao,wanavyojivuniakuwa wahusika wakuu katika kulisha taifahivyo kuonyesha umuhimu wao katika jamii.Ukuwaji wa uzalishaji chakula kwa sasa hauendani na mahitaji ya duniakwani ongezeko la watu ni kubwana uzalishaji chakula badounaonekana upo kwenye kiwango cha chini sana. Hali hii piaimeathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi yanayokuwa kwa kasi kadirisiku zinavyokwenda kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamuzifanywazo pasipo kuwa na tahadhari .
Jumuiko hili litagusia mambo mbalimbali ikiwemo wiki ya Chakuladuniani, ambapo malengo yake ni kuimarisha uzalishaji na kuhakikishaupatikanaji wa chakua salama na cha kutosha,kinachokidhi mahitaji yadunia.Mkutano huu unatoa fursa ya kuaongea kuhusu faida wanayoipatakupitia bajeti ya kilimo katika kukidhi mahitaji ya wazalishaji chakula wadogo Pia itawapa fursa ya wao kuelezea umuhimu wa Serikalikutimiza ahadi yake ya Malabo ya kutenga walau aslimia kumi ya bajeti ya nchi katika sekta ya kilimo.Mambo ya umiliki wa ardhi, upatikanaji wa masoko na pembejeo pia zitakuwa mojawapo ya madazitakazoongelewa. Bila kusahau ushiriki wao katika uundaji nautekelezaji wa sera ya sekta ya kilimo.Hii pia itakuwa ni sehemu ya wazalishaji wa chakula wadogo wadogokupeleka ujumbe kwa Rais Mteule John Joseph Pombe Magufuli kuhusuumuhimu wa kuwekeza kwenye kilimo na kuwapa kipaumbele watanzania wakulima wadogo wadogo kama ushiriki wake wa kuinuakipato na utekelezaji wa sera za kilimo zenye tija kwa wazalishaji wadogo wa chakulaKama ilivyo kwenye uchimbaji wa madini kuwa wachimbaji wadogo wamepewa nafasi na sauti zao kusikika basi hata wakulima wadogo wadogo wapewe kipaumbele kama ilivyo kwenye sekta ya madini.Kilimoni uti wa mgongo tukilee na kukilinda ili tuwe na Taifa lenye uhakika wachakula salama na chakutosha.
|

0 comments:
Post a Comment