Jaji
Kiongozi, Shaban Lila alisema jana kuwa tayari wadau mbalimbali wa haki
jinai wameanza kukutana kuangalia namna ya kuanzisha mahakama hiyo kama
sehemu ya utekejezaji wa ahadi ya Rais.
Akizungumza
katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya kushughulikia mashauri nyeti ya
jinai kwa majaji 12 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alisema juzi walikuwa
na mazungumzo na Wizara ya Katiba na Sheria kuangalia mfumo wa
uendeshaji wa mahakama hiyo.
“Tunaangalia
tuianzishe kama mahakama huru au ifanywe ndani ya muundo wetu wa
mahakama kwa kuipa kipaumbele maalumu. Lakini tunafikiria zaidi kama
ingekuwa ni kitengo maalumu ndani ya Mahakama Kuu kitakachokuwa
kikishughulikia mafisadi,” alisema Jaji Lila.
Hata
hivyo, Jaji Lila hakutaja muda maalumu utakaotumika kumaliza mchakato
wa kuanzisha mahakama hiyo, huku akisema unahusisha wadau wengi na
unyeti wake unahitaji maandalizi makubwa.
Jaji
huyo bila kutaja takwimu, alieleza kuwa kesi za makosa makubwa ya jinai
zinaongezeka nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa zile
zinazohusu utakatishaji fedha, ugaidi, usafirishaji wa dawa za kulevya,
usafirishaji wa nyara za Serikali hasa wanyama hai na mazao yake na
ufisadi.
Balozi
wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alimpongeza Rais Magufuli kwa
kuonyesha msimamo wa kupambana na makosa ya jinai yakiwamo ya dawa ya
kulevya, usafirishaji wa nyara za Serikali na utakatishaji fedha.
“Nilikuwa
nimeketi bungeni namsikiliza Rais siku alipokuwa akilihutubia Bunge,
japo hotuba yake ilikuwa kwa Kiswahili lakini nilipata faraja kubwa
nilipomuona akiwa mkali katika masuala hayo,” alisema Balozi Melrose.
Hii safi sana na hapa inabidi marais waliopita kina Mwinyi, Mkapa, na JK wakamatwe na kuchukuliwa hatua maana hawa ndiyo walioanzisha usanii Tanzania kwa kuifirisi nchi na wizi wa wazi wazi huku wananchi tukihangaika kwa kukosa kunufaika na taifa letu. Wakamatwe hawa marais na wakionekana na makosa ambayo wanayo for sure basi ni kunyongwa tu tena hadharani ili kuwashikisha adabu.
ReplyDelete