Monday, November 30, 2015

Mwenyekiti Bodi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk Agustine Mahiga amewataka wahitimu wa chuo kikuu hicho kujiongezea Elimu ya Ufundi na ujuzi katika fani mbalimbali, ili kuwa na fursa za ajira na kupanua wigo wa ujasiriamali.

Balozi Mahiga alitoa kauli katika Mahafali ya Sita yaliyofanyika Udom kwenye Ukumbi wa Chimwaga chuoni hapo.

Aliwapongeza wahitimu wote kwa kufanya vizuri zaidi na kupata Shahada zenye Sifa bora zaidi ya wengine

Pia aliwasihi aliwasihi wanafunzi waliojiunga na chuo hicho mwaka huu wa masomo kutumia fursa nyingi za kisheria kujadili mambo yanayowakwaza na kuboresha mazingira yao ya masomo na makazi.

Makamu wa mkuu wa chuo hicho, Proffesor Idrisa Kikula alisema wahitimu 4,136 walihitimu katika Ngazi mbalimbali za masomo ikiwamo Vyeti, Stashahada, Shahada, Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu. Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alijivunia Mafanikio yaliyofikiwa tangu chuo hicho kwa kusimamiwa misingi ya taaluma.


0 comments:

Post a Comment