Orodha ya wasanii wa kimataifa watakaotumbuiza kwenye tamasha la la BET Experience Africa linalotarajiwa kufanyika December 12, 2015 jijini Johannesburg, Afrika Kusini inazidi kuongezeka.
Muimbaji mkongwe wa Rnb na mshindi wa tuzo ya Grammy, Mary J Blige kutoka Marekani metangazwa kuungana na wasanii wengine waliokuwa wameishatajwa akiwemo staa wetu Diamond Platnumz.
Miongoni mwa hit songs za Mary J. Blige ni pamoja na
‘Family Affair’, ‘No More Drama’ pamoja na ‘Be Without You’.
Wasanii wengine kutoka Afrika watakaoshare jukwaa moja na staa huyo ni AKA , Flavour , Nathi, DJ Euphonik na Black Motion.
Tamar Braxton kutoka Marekani pia alikuwa ametajwa
kutumbuiza, lakini wiki hii waandaaji wa tamasha hilo walisema kuna
uwezekano asihudhurie kama ilivyotangazwa awali kutokana na kuruhusiwa
kutoka hospitali hivi karibuni alikokuwa akitibiwa.
Tamasha hilo la siku nzima litahusisha burudani mbalimbali ikiwemo muziki, vichekesho, mitindo, michezo na vingine.
0 comments:
Post a Comment