Posted by Williammalecela.com on Friday, November 27, 2015
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.
Nehemia Kyando Mchechu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari
Novemba 26, 2015 Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa mauzo ya nyumba katika mradi mpya wa Seven Eleven (711)
ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam (kulia) Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hamad Abdallah.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu
akiwaonesha waandishi wa habari michoro ya ramani ya mradi wa nyumba
ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza kwa umakini, Bw. Nehemia Kyando Mchechu.
Mkutano ukiendelea.
Waandishi wa habari wakitembelea katika eneo la ujenzi huo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Ujenzi ukiendelea
Ujenzi ukiendelea
Waandshi
wa habari pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa
wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.
Nehemia Kyando Mchechu wakati wa uzinduzi huo.**************Na Philemon Solomon Fullshangweblog SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) lazindua mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe ,ambapo ujenzi huo ulianza Januari 2015.Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.
Nehemia Kyando Mchechu alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa
kukamilika ifikapo Desemba 2018 ,ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya
kuanza ujenzi. Mradi huo una ukubwa wa mita za mraba 111,842.90 ambao
unatarajiwa kugarimu kiasi cha zaidi ya Sh 187, 927, 105,500 mpaka
utakapomalizika .Pia ikumbukwe kuwa mradi huu ni
seemu ya mji mpya wa kisasa (Satellite City) unajengwa hapa ,mradi huu
upo katika eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko mita
chache kutoka fuko za bahari ya Hindi pia karibu na maeneo muhimu kama
Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay, Morocco na Mikocheni mradi huu una
jumla ya nyumba 422 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo nane tofauti ya
ghorofa 18 kila moja, ukiwa na huduma zote muhimu za kijamii.pia
kutakuwepo na seemu ya maduka makubwa kwa ajili ya wakazi na maeneo ya
jirani”Alisema Mchechu.
0 comments:
Post a Comment