Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amemuomba mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich muda zaidi wa kukijenga kikosi chake kufuatia kuanza msimu wa 2015/2016 vibaya.
Taarifa zinasema Mourinho amefikia uamuzi wa kumuomba muda tajiri huyo kutokana na matokeo anayopata na anachohitaji ni muda ili asubiri dirisha la usajiri la January.
Taarifa hizo zinasema Mourinho anataka kufanya usajili kwa kutoa wachezaji ambao anaona hawana uwezo wa kucheza kwenye kikosi chake na kuingiza wachezaji.
Pamoja na hayo taarifa zinasema tajiri wa timu hiyo Abramovich amesema kuwa bado anamuhitaji kocha huyo na anaamini atakibadili kikosi hicho na kurudi katika makali kama ya msimu uliopita ambayo yaliwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Wingereza.
Chelsea kwa msimu wa 2015/2016 imeanza msimu vibaya ambapo katika michezo 12 ya ligi kuu ya Wingereza imeyocheza mpaka sasa imeambulia alama 11 kwa kupoteza michezo 7, kushinda 3 na kutoa sare 2.

0 comments:
Post a Comment