Kikosi cha New York City.
Mchezaji wa zamani wa Arsenal na kocha wa timu kukuzia vipaji ya vijana ya Manchester City, Patrick Vieira ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya New York City inayoshiriki ligi kuu ya nchini Marekani MSL.
Uteuzi wa Vieira umekuja ikiwa ni siku sita (6) tangu kutimuliwa kazi aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jason Kreis.
Vieira ambae anaiongoza timu ya vijana kuangalia maendeleo ya vijana alijiunga na timu hiyo 2013 na katika miaka yake miwili ya kuongoza timu hiyo ameweza kupata mafanikio ikiwepo kuiwezesha kutwaa ubingwa wa kombe la ligi kuu ya kimataifa kwa upande wa vijana na mpaka sasa inaongoza kundi lake katika kombe la Uefa la vijana.
Akizungumza uteuzi huo Vieira amesema ni jambo la furaha kwake kuteuliwa kocha mkuu na ameushukuru uongozi wa Manchester City pamoja na mashabiki kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi chote alichokuwa katika klabu hiyo.
“Ni furaha kupata nafasi ya kuwa kocha mkuu wa New York City. Kufanya kazi na Claudio Reyna na Rob Vartughian pamoja na hamasa kutoka kwa mashabiki kunafanya ufanyaji wa kazi kwa mwalimu kuwa mzuri zaidi,
” Ninamshukuru kila mtu ndani ya klabu ya Manchester City na zaidi kwa Brian Marwood, kwa makocha wenzangu nakwa mashabiki ambao walihakikisha mambo yanakuwa sawa katika kuiongoza timu ya vijana, uwajibikaji wao katika kazi umenifanya niwe na wakati mzuri katika maisha yangu ya ukocha katika timu hii,” alisema Vieira.
Akizungumzia timu aliyokuwa anaiongoza amesema “Ni wachezaji wazuri na watu wazuri, nawafahamu vizuri na kama naamini watazidi kwenda mbele zaidi katika maisha yao ya soka”
Aidha kocha huyo anatarajiwa kuanza majukumu yake ya ukocha kukinoa kikosi hicho cha New York City Januari 1 mwakani.


0 comments:
Post a Comment