Monday, November 16, 2015

AWACHA KWA CHAFUKA! WATUPIANA MATUSI YA NGUONI.
KUMBE MARIAM MSABAHA MCHAGA???
16th Nov 2015 02:10 am
Wanakisima Jinamizi la ukabila juu ya upatikanaji wabunge wa viti maalum ndani ya BAWACHA bado laendelea kulitesa baraza hilo linalo ongozwa na Halima Mdee.
Hamida anayetajwa katika majibizano haya ya whatspp ndio kiongozi pekee wa BAWACHA ambaye si mbunge wa viti maalum. Hamida ni makamu mwenyekiti wa BAWACHA upande wa Zanzibar na alipata nafasi hiyo baada ya kumshinda Maryam Msabaha.
Inasemekana ama waweza kusema kuna tuhuma kuwa kigezo kikubwa cha kupata ubunge wa viti maalum ndani ya CHADEMA aidha uwe karibu na viongozi wa kitaifa chama hicho(kimapenz) au uwe mchaga.
Maryam Msabaha ni mchaga, na kama majibizano hayo yanavyo jieleza, kwao kaskazini kwanza Zanzibar baadae!
BAWACHA wanatuhumiana wenyewe kwa wenyewe, BAWACHA hawapatani, BAWACHA ukabila unawatafuna, BAWACHA viti maalum vimewavuruga! BAWACHA haijatulia, BAWACHA yahitaji kupepewa!
Baada ya kuvuana nguo katika group lao la whatspp wakaamua kulifunga na kufungua lingine ambalo wale wenye vurugu hawatahushwa! Inasemekana kila makundi mahasimu kila moja sasa limefungua kundi lake, makundi ambayo yabahusisha baadhi ya viongoz wa waandamizi wa BAWACHA na wabunge wa viti maalum.
BAWACHA waliotemwa wana hasira, sababu kuna uwezekano mkubwa uchaguzi wa mwaka 2020 tutafanya chini ya katiba mpya, katiba ambayo haitakuwa na viti maalum, wanawake watatakiwa kwenda kugombea majimboni, hivyo kwa wale wanawake waoga wa kwenda jimboni mwaka huu ilikuwa ndio turufu yao mwisho!
Kwahivyo waweza kugundua hasira zao zimesababishwa na tuhuma za ukabila, lakini pia nafasi hizo hazitakuwepo tena mwaka 2020. Binafsi naomba heri mwaka 2020 tupate katiba mpya ili dada zetu waponyeke na viboko vya viongozi wenye sauti katika vyama vya siasa!
Wanakisima tuendelee kuwa pamoja, hiv karibuni nitawapa lingine lililotokea BAVICHA na UWT, nina fuatilia uthibitisho tu wa habari zenyewe, na nikipata sitaacha kuwajuza watu wangu.

0 comments:

Post a Comment