klabu ya soka ya Sunderland imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza wakiwa Ugenini baada ya kuifunga Crystal Palace 1-0.
Bao pekee la ushindi la Sunderland lilifungwa na Jermain Defoe Ushindi ambao umewaweka Sunderland katika Nafasi ya 18 wakiwa na Pointi 9 baada ya kucheza Mechi 13.
Ligi ya England inatarajia kuendelea tena Jumamosi ya Novemba 28 kwa michezo mbalimbali ambapo, Aston Villa watakuwa wenyeji wa Watford.
Bournemouth watawaalika Everton , Crystal Palace watawakaribisha Newcastle, Man City watakuwa wenyeji wa Southampton , Sunderland wataumana na Stoke Huku Leicester city wakiwakaribisha Man United.
0 comments:
Post a Comment