Habari zenu wanajamii wa kitanzania hasa wale wapenda soka. Nimekaa
nikafikiri sana na kupata muarobaini ambao ukitumika ipasavyo kwa
mipango madhubuti basi tunaweza kulikaribia lengo au kulifikia lengo
kabisa katika kupiga hatua ya kuzalisha vipaji madhubuti vya soka.
TFF ndiyo iliyopewa dhamana ya kusimamia soka pamoja na kutoa dira ya
muda mfupi na muda mrefu ya muelekeo wa soka la faifa letu.
Kwa mipango ya muda mfupi, TFF inatakiwa kuweka sheria kali kwa kila
club inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania kuwa na timu mbili za vijana
nikimaanisha U17 pamoja na U21.
Hii itasaidia kuzalisha vipaji endelevu kila kukicha na kuzipunguzia
timu gharama ya kusajili wachezaji kwabei ghali, badala yake hizo
gharama kuelekezwa kwa timu hizo za vijana kupata vifaa na elimu ya kuwa
professional kwenye kazi hii ya mpira.
Pia ili kuona timu hizi za vijana zinakuwa active na sio jina tu, TFF
waandae ligi kuuza za U17 na U21 ambazo zitashirikisha timu ambazo timu
kubwa zao zipo ligi kuu. Tunaona mataifa yaliyoendelea kama Uingereza,
Spain na Germany wamefanikiwa sana kwenye hili na kufanya nchi hizo
kupiga hatua kisoka.
Pia ligi hizi za vijana zikiwa zinafanyika zitampa wasaa mzuri kocha
wa vijana kuona vipaji na kuchagua wachezaji kwa ajili ya timu za taifa
za vijana ambazo ndiyo zitakuwa zalisho bora kwa senior national team.
Kwakweli watanzania wenzangu zoezi hili likifanyika kwa ufasaha
kabisa ni lazima tutawapata akina Samata wengi sana, pia vijana
wakiwekwa kwenye timu wakiwa wadogo hata nidhamu ya uwanjani na ya nje
ya uwanja itakuwa ni rahisi kufundishwa na kuweza kukua nayo kuliko
kuanza kuwafundisha wakiwa wakubwa tayari, siri kubwa ya wachezaji
kufanikiwa ni nidhamu binafsi ya nje na ndani ya uwanja.
Pia vilabu vitapata faida pale wanapopata majeruhi wengi kwenye clubs
zao, watakuwa na uwezo wa kuchukua vijana wao na kuwatumia kwenye ligi
mara moja (Kama sheria ya TFF inaruhusu).
Kwa mipango ya muda mrefu TFF kama chombo kilichopewa dhamana ya
kusimamia soka nchini wanatakiwa waje na mipango madhubuti ya kuweza
kutuvusha, na mojawapo ni kuzalisha wakufunzi wengi wa soka ambao
watasambazwa nchi nzima kufundisha vijana wadogo kabisa.
Hii itafanyikaje ilhali tuna Accademy chache nchini? Kwa kuanzia
inabidi tuanzie mashuleni kuanzia shule za msingi, kila shule ya msingi
inatakiwa iwe na mwalimu aliyesomea mpira na siyo yule anayeangalia tu
na kuja na mambo yake ambayo hayana program.
Kwahiyo TFF kwa kushirikiana na serikali wanatakiwa waweke mwalimu wa
soka kwa kila shule ya msingi anayepata nafasi ya kufundisha soka na
nidhamu kuanzia umri mdogo mashuleni (Wizara ya Elimu na michezo ni
wadau wakubwa kwenye hili). Lakini sio kwa kuishia hapo tu pia kwa ngazi
ya shule za secondary waalimu wa soka wanahitajika pia.
Kumbuka hii ni mipango ya muda mrefu siyo ya muda mfupi kwahiyo
matunda yake tutaanza yaona baada ya miaka 10+, tunatakiwa tuwe
wavumilivu sana ikiwa tunataka kuvuka hapa tulipo angalau tukipata
waalimu wa soka kama1000 utakuwa ni mwanzo mzuri sana kwa maendeleo ya
soka la nchi yetu kwa miaka 10+ ijayo. Na wakufunzi hao wanatakiwa wawe
na agenda moja ya taifa na sio kila mmoja kuwa na program yake, lengo
liwe moja nchi nzima (Germany wamefanikiwa sana kwa hili tunaweza
kuwatumia kama case study).
Lakini tukiwa tunatumia hizi shule zetu za kawaida hapohapo TFF
inatakiwa iweke vipaombele kwenye kujenga Academy zake na pia kuviwekea
vilabu vya soka masharti ya kushiriki ligi kuu ikiwa ni pamoja na kuwa
na Academy inayoeleweka ndani ya miaka 10 ijayo (Tuliona mpango wa
Sunderland kutaka kuisaidia Simba ila hatujui ulipofia mpango huo).
Timu kama Azam imefanikiwa kwa hilo chini ya miaka 10 basi hata hawa wengine wakiwekewa masharti hayo wanaweza kufanya.
Kila jambo lolote zuri linahitaji gharama kwahiyo wasimamizi wa mpira
wanatakiwa wafanye plan nzuri na kuandaa budget yenye tija kwa
kushirikiana na serikali waweze kutekeleza haya na kutafuta wafadhili
wenye nia ya kuibua vipaji nchini ambao najua wapo wengi tu watu wenye
nia njema na soka la taifa hili.
Tukumbuke pia uki-invest sehemu kwa pesa nyingi pia outcome yake huwa
inakuwa kubwa kama ukisimamia vizuri. Football ni biashara kubwa sana
kwa nchi za wenzetu na inachangia asilimia kubwa sana ya pato la taifa
kwa nchi hizo.
Ndugu zangu watanzania, wazungu wanasema “this is not a rocket
science” na hakuna shortcut kwenye hili lazima tufate procedure na
kupata wataalamu wazawa wa kusimamia haya kwa ukamilifu.
Tuache majungu na kuishi kwa mazoea kwamba tutafanikiwa, maamuzi
magumu ni lazima yafanyike ili tuvuke. Tutaendelea kwenye makala
nyingine kwa kuona mifano hai ya nchi zilizopiga hatua walifanyaje.
0 comments:
Post a Comment