Chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kimethibitisha kuwa mwenyeji
wa mashindano makubwa ya vilabu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
KAGAME CUP, ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi wa July, 2015.
Mkurugenzi wa ufundi wa ZFA Massoud Attai amethibitisha kuwa Zanzibar
watakuwa wenyeji kuandaa mashindano hayo ambapo walipelekea maombi yao
kwa CECAFA kwa kutaka kuwa wenyeji na CECAFA wamekubali Zanzibar kuandaa
michuano hiyo mwakani (2016) na kwasasa maandalizi yameshaanza maana
Baraza la michezo tayari wameshapokea barua ya kuwa Zanzibar ni wenyeji
wa michuano hiyo.
“Ni kweli Zanzibar tumepeleka maombi yetu kwa CECAFA kuwa mwenyeji na
tayari wameshatukubalia, kwaiyo yatafanyika mwakani bila wasiwasi
wowote”, amesema Attai.
Katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika ndani ya visiwa vya
zanziabar ambapo timu ya Mafunzo na JKU ndiyo bingwa na makamu bingwa wa
ligi kuu ya Zanzibar msimu wa 2014-2015 ndio watakaowakilisha Zanzibar,
lakini pia hii si mara ya kwanza kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa michuano
hiyo ambapo waliwahi kuwa wenyeji miaka mingi sana kama mwaka 1985 na
1990 na mashindano yakachezwa kwa utulivu.
0 comments:
Post a Comment