Nyingine ni Wizara Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Nchi.
Wakati
kukiwa na taarifa kwamba Rais Dk. John Magufuli, anatarajia kupunguza
karibu nusu ya wizara zilizokuwapo kwenye Serikali ya Awamu ya Nne,
imefahamika kuwa wizara zinazolengwa ni zile zilizopo Ofisi ya Rais,
Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Chanzo
kimoja kutoka serikalini kimeiambia Nipashe jana kuwa wizara hizo
zitaunganishwa kwenye wizara mpya zitakazoanzishwa na Rais ambaye
ameweka mkakati wa kuwa na baraza dogo la mawaziri.
Wizara
zinazotajwa kufyekwa ni Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji,
Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais
Mahusiano na Uratibu, Wizara Ofisi ya Waziri Mkuu na Sera, Uratibu na
Bunge.
Nyingine
ni Wizara Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano, Wizara ya Nchi, Ofisi Makamu wa Rais Mazingira na Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Kadhalika,
katika mabadiliko hayo, wizara nyingine zitaguswa ili kufikia malengo
ya kubakia na wizara chache kutimiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya
Tano kubana matumizi na kuinua maisha ya Watanzania.
Chanzo
hicho kimebainisha kuwa Rais Dk. Magufuli atalitangaza Baraza la
Mawaziri ndani ya wiki hii ingawa bado kumekuwa na usiri wa siku halisi
atakayotangaza.
Serikali
ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, ilimaliza muda wake Novemba 5,
mwaka huu ikiwa na wizara 30. Vile vile, alipoingia kwa mara ya kwanza
mwaka 2005, Rais Kikwete alikuwa na serikali kubwa yenye mawaziri na
naibu wao zaidi ya 60.
Rais
Magufuli aliyeapishwa Novemba 5, mwaka huu, tayari ameshamteua Mbunge
wa Ruangwa, Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa serikali yake na Ijumaa
iliyopita alizindua rasmi Bunge la 11.
Juzi,
chanzo kimoja kililiambia Nipashe kuwa tayari Rais Magufuli kwa
kushirikiana na wasaidizi wake, ameshakamilisha sehemu kubwa ya mchakato
wa kuunda baraza lake la mawaziri na kwamba kinachosubiriwa sasa ni
kulitangaza wakati wowote kuanzia sasa.
NIPASHE

0 comments:
Post a Comment