CHAMA cha
ACT- Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, umeandaa maandamano ya kumuunga
mkono Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano yake dhidi ya rushwa,
ufisadi na kusimamia ukusanyaji kodi kama ilani ya chama hicho
inavyosema.
Katibu wa
chama hicho, mkoani humo, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, aliyasema hayo
katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa,
wamemuandikia barua Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadiki ili kumuomba
ayapokee maandamano hayo ya amani.
"Tumepanga
kufanya maandamano hayo Desemba 16 mwaka huu, tukianzia katika ofisi
zetu za Mkoa eneo la Keko Maduka Mawili na kuishia Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa, Ilala Boma," alisema.
Alisema
lengo lingine la kufanya maandamano hayo ni kumtaka Rais asimamie
uongozi bora wenye lengo la kuirudisha nchi kwenye misingi iliyoasisiwa
na wazee Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume.
Aliongeza
kuwa, ilani ya chama chao ukurasa wa saba inaelezea ndoto ya
ACT-Wazalendo ni kuona Taifa linajitegemea kiuchumi, kiutamaduni,
kudumisha usawa, ustawi wa jamii, uwajibikaji, demokrasia, uongozi bora.
Mhandisi
Ngulangwa alisema chama hicho kinaamini kuwa, mambo hayo yatatekelezwa
vizuri kama nchi itajiwekea miiko ya uongozi kama inavyoelezwa na Azimio
la Tabora lililohuishwa kutoka Azimio la Arusha.
"Lengo
lingine ni kumuomba Rais ahakikishe nchi kupitia mamlaka husika,
inasimamia mfumo wa matumizi ya fedha kama inavyosema katika ilani ya
chama chetu ukurasa wa 23.
"Hata
hivyo, yote hayatakuwa na maana kama mfumo wa fedha kupitia benki
utakuwa umeshikwa na wageni kwani nchi yetu haiwezi kuendelea ikiwa
benki kubwa zitakuwa zimebinafsishwa," alisema.
Alisema
uanzishaji benki uliofanyika mwaka 1967 na kuundwa kwa Benki ya Taifa ya
Biashara (NBC), Benki ya Nyumba na Benki ya Maendeleo Vijijini ni
maamuzi ya msingi kwa maendeleo ya nchi

0 comments:
Post a Comment